Connect with us

General News

Monkeypox imeathiri 1,400 Afrika – WHO – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Monkeypox imeathiri 1,400 Afrika – WHO – Taifa Leo

Monkeypox imeathiri 1,400 Afrika – WHO

NA MASHIRIKA

GENEVA, Uswisi

VISA 1,400 vya ndui ya nyani (monkeypox) vimeripotiwa katika nchi saba za Afrika mwaka huu, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Visa hivyo vimeripotiwa katika nchi za Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Liberia, Nigeria, Congo-Brazzaville na Sierra Leone.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa, linasema kuwa visa vya monkeypox vilivyothibitishwa barani Afrika mwaka huu ni vichache ikilinganishwa na mwaka 2021. WHO imeonya kuwa ugonjwa huo sasa unasambaa kwa kasi ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Nigeria imerekodi visa 21 vya maradhi hayo katika majimbo tisa na mtu mmoja ameaga dunia tangu Januari 2022.

Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mgonjwa wa umri wa miaka 40 aliyefariki kutokana na ndui ya nyani, alikuwa na maradhi mengineyo.

Visa vingi vya maradhi hayo nchini Nigeria vilishuhudiwa mwezi jana.

Kituo cha Kukabiliana na Maradhi nchini Nigeria (NCDC), kimewataka raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuzingatia ushauri unaotolewa na wizara ya Afya kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Ugonjwa huo umezua hofu duniani baada ya kusambaa kwa kasi katika nchi za Ulaya na Amerika.

Amerika imethibitisha takribani visa 16 huku Uingereza ikiripoti visa zaidi ya 180. Serikali ya Uingereza imeshauri waathiriwa wa ndui ya nyani kujiepusha na ngono ili kuepuka kuusambaza zaidi.

Uingereza pia imewataka waathiriwa kujitenga na watu wengine kwa wiki tatu mara baada ya kuanza kuona dalili za ugonjwa huo.

Serikali ya nchi hiyo pia imewashauri waathiriwa waliopona kutumia kinga kama vile mipira ya kondomu wanaposhiriki tendo la ndoa.

Ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo 1970 barani Afrika. Miaka ya 1980 ulionekana kuangamizwa lakini ukaibuka tena baada ya miaka michache.

Visa kadhaa vimekuwa vikiripotiwa katika mataifa 10 ya Afrika haswa kwenye vijiji vilivyo maeneo ya misituni.

Mnamo 2003, kulitokea mlipuko nchini Amerika, mara ya kwanza ugonjwa huo kuonekana nje ya Afrika. Wagonjwa walipata ugonjwa huo kutokana na kutangamana na mbwa mwitu.

Dalili za awali za ugonjwa huo ni joto jingi mwilini, kuumwa na kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo, maumivu ya misuli na udhaifu wa mwili. Upele unaweza kutokea, mara nyingi huanzia usoni, kisha kuenea kwa sehemu nyingine za mwili, kwa kawaida viganja vya mikono na nyayo za miguu.

Shirika la WHO linasema kuwa ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa hivyo hakuna haja ya ulimwengu kuwa na wasiwasi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending