Connect with us

General News

Mpenzi wa zamani ni sawa na kiporo, hakiliki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mpenzi wa zamani ni sawa na kiporo, hakiliki – Taifa Leo

BAHARI YA MAPENZI: Mpenzi wa zamani ni sawa na kiporo, hakiliki

NA SIZARINA HAMISI

KUPASHA viporo katika mapenzi ama ndoa ni jambo ambalo limekuwa linafanyika na wengi.

Ingawa pia wapo wengi wanaoendeleza urafiki na wapenzi wao wa zamani bila ya kurudi tena kwenye mapenzi. Kwa upande mwingine wapo ambao suala la urafiki huwashinda na kujipata wanakumbushiana mapenzi yao ya zamani.

Unapoingia kwenye ndoa, inamaanisha kwamba maisha yenu pamoja yanatakiwa yawahusishe ninyi wawili. Na mara nyingi iwapo ndoa itakuwa imetulia, haina misukosuko, ni aghalabu kupata wanandoa wakirudiana ama kuanzisha mawasiliano na wapenzi wa zamani. Iwapo utampenda, kumtunza, kumheshimu na kutimiza mahitaji yote ya muhimu ya mwenzako suala la kuwasiliana na yule aliyepita huwa na nafasi ndogo sana. Lakini hali inapokuwa tofauti, aidha umnyanyase mwenzako, maisha yawatandike hadi mshindwe kuhema.

Siku zote kuwa na uhusiano wa kirafiki na mpenzi wa zamani huwa ni jambo lenye utata mwingi. Kwani kama huyo unayetaka kuwa rafiki alikuwa mpenzi wako na sehemu ya maisha yako, ni kawaida ya kibinadamu kutaka kuendelea kuhusiana naye, hasa kama hamkuachana kwa ubaya. Na unapoingia kwenye ndoa mambo yanaweza kukanganyika zaidi iwapo utaamua kuendelea na urafiki na mpenzio wa zamani.

Ukweli mwingine ni kwamba wengi wanaodai ni marafiki na wapenzi wao wa zamani mara nyingi urafiki huo huzama zaidi ya urafiki wa kawaida, masuala ya hisia huwa hayatabiriki na hayaeleweki wakati mwingine.

Kunaweza kuwa na tofauti iwapo huyo mhusika ulikuwa naye rafiki kwa muda mrefu hata kabla ya kuingia kwenye ndoa na hamkuwa na mahusiano ya ukaribu ya kimapenzi.

Muhimu ni, umeamua kuendelea na urafiki na mpenzi wako wa zamani, kuwa muwazi kwa mwenzako katika ndoa.

Isije ikawa kwamba unakutana na huyo rafiki yako kwa siri na unamficha mume ama mkeo kwamba unakutana na mpenzio wa zamani ambaye sasa amekuwa rafiki. Katika yote, ndoa yenu inatakiwa iwe kipaumbele kuliko urafiki.

Weka mambo hadharani na umweleze mwenzako. Iwapo mtakubaliana ni sawa lakini pia uheshimu uamuzi wa mwenzako iwapo ataona urafiki wenu una walakini.

Katika yote, ndoa yenu inatakiwa iwe kipaumbele kuliko urafiki na wapenzi wa zamani. Urafiki na mpenzi wako wa zamani haifai kuwa sehemu ya uhusiano katika ndoa yako.

Yaliyopita ni vyema yabaki yalikopita na huna budi ugange yale yaliyopo ambayo ni uhusiano na mwenzako katika ndoa.

[email protected]

NI kawaida kusikia baadhi ya watu walio katika ndoa wakisema kwamba wangali marafiki na wapenzi wao wa zamani.

Unasikia mtu akimwambia mkewe au mumewe kwamba japo aliachana na mpenzi wake wa zamani wangali marafiki. Baadhi yao huwa wanaongeza kusema kuwa “ wangali marafiki wazuri” na wapenzi wao wa zamani kiasi cha kusaidiana, kukutana na kujivinjari pamoja wakisisitiza kuwa hakuna cha ziada kati yao.

Kusema “hakuna cha ziada” huwa wanamaanisha huwa hawana hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao wa zamani. Hata hivyo, ni mtu mjinga kupindukia anayeweza kuamini kwamba hisia za mapenzi haziwezi kuchipuka upya kati ya watu waliokuwa wapenzi.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba mtu akichangamkia mpenzi wa zamani bado huwa anamtamani. Inasemwa kuwa hata wakitengana, watu wawili waliojifunika blanketi moja wanaweza kurambishana asali wakikutana chemba.

Hivyo basi, kuruhusu mke au mume wako kukutana na mpenzi wake wa zamani ni sawa na kumpa ruhusa ya kumrudia. Watu wengi wamekuwa wakivunja ndoa zao kwa sababu ya kudumisha mawasiliano na wachumba wao wa zamani badala ya kuzingatia kujenga ndoa zao.

Unapata mtu akitumia muda mrefu kuwasiliana na mchumba wake wa zamani, muda ambao angekuwa akitumia kumdekeza mume au mke wake. Kufanya hivi ni kualika balaa.

Namjua mwanadada aliyezaa na mpenzi wake wa zamani akiwa kwa ndoa japo alikuwa akimdaganya mumewe kwamba kilichokuwa kimebaki kati yake na mwanamume huyo ni urafiki wa kawaida pekee. Mumewe aligundua na kumtaliki kisha mpenzi wa zamani aliyemzalisha akamhepa.

Ukioa au ukiolewa, unafaa kuweka mipaka kati yako na wapenzi wako wa zamani kwa manufaa ya ndoa yako. Hata kama mtakuwa marafiki hasa kwa wale wanaoachana bila taharuki, epuka mazoea ya kuwasiliana au kukutana ili usifanye mume au mkeo kukushuku.

Binadamu ana wivu hasa pale kuna hatari ya mtu mwingine kuchovya asali yake na kama nilivyotangulia kusema, chochote kinawezekana watu waliokuwa wapenzi wakikutana. Ikiwa ni vigumu kumwepuka mpenzi wako wa zamani, msikutane faraghani, usimtembelee kwake na pia usikubali akutembelee kwako kwa kuwa kufanya hivi ni kumimina sumu katika ndoa yako.

Hata kama haukuachana na mpenzi wako wa zamani kwa ubaya, anaweza kuleta balaa katika ndoa yako. Hakuna mtu anayeweza kuvumilia mke au mume wake akichangamkia mpenzi wake wa zamani. Labda kwa dawa.

Hakikisha mpenzi wako wa zamani hana namba yako ya simu. Ni muhimu kuwa mwangalifu kwa sababu mtu aliyeachwa anaweza kupalilia urafiki ili kuharibia aliyemuacha ndoa yake. Ukiacha mtu na asisitize muwe marafiki wa kawaida, fikiria mara mbili kwa sababu anaweza kuwa na nia fiche.

Hakuna mtu anayeweza kuamini kwamba mkewe au mumewe ana urafiki wa kawaida na mpenzi wake wa zamani. Ili kulinda ndoa yako na hata uhusiano wako wa mapenzi, epuka kabisa urafiki wa aina hii kwa sababu kusema kweli, ni hadaa tupu.

[email protected]