– Nancy Onyancha pamoja na mumewe Joab Mwaura walikuwa miongoni mwa wanahabari 100 waliofutwa kazi na K24 TV
– Wiki moja baadaye, Nancy ambaye ni mtangazaji wa lugha ya Kiswahili, amepata kazi tena katika runinga ya Switch TV
– Nancy na Mwaura wanasemekana kuzindua shirika lao la utangazaji maarufu kama ‘Sauti Tajika’
Mtangazaji Nancy Onyancha amepata kazi katika runinga ya Switch TV, majuma mawili tu baada ya kufutwa kazi kutoka runinga ya K24 inayomilikiwa na shirika la Media Max.
Nancy alitangaza habari hiyo njema kupitia mitandao ya kijamii ambapo alimshukuru Mungu kwa kumfungulia mlango mwingine.