Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi amefanya mkutano wa mashauriano na baadhi ya viongozi kutoka eneo la Mlima Kenya
Mudavadi ameshatangaza azma yake ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
” Nilifanya mkutano na baadhi ya viongozi kutoka Nyeri, tulijadili maswala kadhaa yanayowaathiri wakazi wa kaunti hiyo ikiwemo changamoto wanazopitia wakulima wa majani chai na kahawa,” Alisema Mudavadi.