Connect with us

General News

Mvua nyepesi kushuhudiwa nchini hadi Ijumaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mvua nyepesi kushuhudiwa nchini hadi Ijumaa – Taifa Leo

Mvua nyepesi kushuhudiwa nchini hadi Ijumaa

Na CHARLES WASONGA

IDARA ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchi imetangaza kuwa maeneo mbalimbali yatashuhudia mvua nyepesi wiki hii.

Kwenye taarifa kwa vyombo habari Jumatatu, Februari 22, 2022, Mkurugenzi Mkuu wa idara hiyo Stella Aura alisema kuwa maeneo ya Kati mwa Kenya, Nairobi, Mlima Kenya, nyanda za juu za Rift Valley na maeneo ya Ziwa Victoria yatashuhudia mvua nyepesi hadi Ijumaa wiki hii.

Maeneo mengine ya nyanda za chini kama vile kaunti za Kitui, Makueni, Machakos na Taita Taveta pia yatashuhudiwa mvua nyakati za jioni.

“Maeneo mengine ya Pwani pia yatashuhudia mvua za hapa na pale,” akasema Bi Aura.

“Hata hivyo, maeneo mengine ya nchi yataendelea kushuhudia hali ya kiangazi katika mwezi huu wa Februari na mapema mwezi wa Machi,” akaongeza.

Bi Aura alisema jua kali na anga kavu pia inatarajiwa kushuhudiwa katika maeneo mengine nchini Kenya,” akaongeza Bi Aura.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo alisema mvua inayoshuhudiwa sasa sio sehemu ya mvua ya masika inayotarajia kuanza kushuhudiwa nchini mwishoni mwa mwezi Machi.

Maeneo ya Kaskazini mwa Kenya yanaendelea kukabiliwa na makali ya njaa kutokana na ukosefu wa mvua ya kutosha kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Kulingana na serikali, jumla ya watu 2.3 milioni katika maeneo hayo wanategemea chakula cha msaada huku mifugo wakikufa kwa kukosa lishe na maji.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya mifugo 1.4 milioni imeangamia kutokana na hali ya kiangazi inayoshuhudiwa katika maeneo hayo ya Kaskazini mwa Kenya.

Jamii za wafugaji zimekuwa zikipigana kung’ang’ania lishe na maji katika kaunti za Baringo, Isiolo, Lamu, Marsabiti, Laikipia, Samburu, Marsabit, Wajir na Turkana.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending