Connect with us

General News

Mwanaharakati adai UDF ilimtapeli hela za mchujo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanaharakati adai UDF ilimtapeli hela za mchujo – Taifa Leo

Mwanaharakati adai UDF ilimtapeli hela za mchujo

Na BENSON MATHEKA

Mwanaharakati David Kimengere ambaye ni mwanzilishi wa shirika la kijamii la Sauti ya Mnyonge, anataka waliokuwa viongozi wa chama cha United Democratic Forum ambacho kinara wa Amani National Congress Musalia Mudavadi alitumia kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa 2007 wazimwe kugombea viti kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Bw Kimengere ambaye alirejea nchini mwaka jana baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka kadhaa anadai kwamba chama hicho  kilimtapeli pesa kwenye uchaguzi mkuu wa 2007.

Katika barua aliyoandikia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na msajili wa vyama vya kisiasa, Bw Kimengere anasema chama hicho kilikataa kumrudishia Sh35,000 alizolipa kama ada ya mchujo baada ya kubadilisha nia na kuamua kutosimamisha mgombeaji eneobunge la Othaya  kaunti ya Nyeri.

“Licha ya chama hicho kuahidi kunirudishia pesa hizo hakijawahi kufanya hivyo miaka kumi na mitano baadaye,” asema Bw Kimengere.

Anasema juhudi zake za kutaka chama hicho kumpa haki yake zimegonga mwamba hata baada ya aliyekuwa katibu wake mkuu Petronila Were kufahamisha msajili wa vyama kuwa kingemrudishia pesa hizo.

“Ni maoni yangu kwamba waliokuwa maafisa wa chama hicho wanafaa kuzuiwa kushiriki chaguzi zijazo kwa kukiuka maadili,” alisema.