Connect with us

General News

Mwanaharakati awasilisha kesi akitaka DPP ashtakiwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanaharakati awasilisha kesi akitaka DPP ashtakiwe – Taifa Leo

Mwanaharakati awasilisha kesi akitaka DPP ashtakiwe

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAHARAKATI Memba Ocharo amewasilisha kesi katika mahakama ya ajira (ELRC) akiomba tume ya kupambana na ufisadi nchini (EACC) imchunguze Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji na kumfungulia mashtaka kwa kutumia mamlaka ya afisi yake vibaya.

Katika kesi hiyo Bw Ocharo, kupitia kwa mawakili Danstan Omari na Shadrack Wamboi anadai Haji alitangaza nafasi za kazi na kuwaorodhesha watu kutoka jamii moja kuhojiwa kwa lengo la kuajiriwa.

Bw Omari anasema Bw Haji amekaidi vifungu kadhaa vya katiba vikiwamo nambari 73 (2), 232 na Sheria nambari 3 na 8 za maadili na uongozi bora.

“Jinsi DPP Haji anavyowashtaki watumishi wakuu serikalini ikiwa ni pamoja na magavana, mawaziri na wafanyakazi wa ngazi za chini serikalini ndivyo atakavyoshtakiwa na kubanduliwa afisini,” asema Bw Omari.

Na wakati huo huo Bw Omari amesema afisi ya DPP kisheria haina mamlaka ya kuwafanyia wasaka ajira mahojiano.

“Jukumu la kuwahoji wasakao ajira ni la tume ya kuajiri watumishi wa umma (PSC) na kamwe afisi ya DPP haijapewa idhini ya kuajiri,” alisema Bw Omari.

Wakili huyo anasema sheria imeipa PSC na tume nyinyine 13 uwezo wa kuhoji maafisa watakaohudumu na afisi ya DPP sio mojawapo ya hizo.

Pia Bw Omari amesema idara nyingine iliyopewa mamlaka ya kuhoji na kuajiri ni afisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.

Wakili huyo amelalamika kuwa Haji amekaidi sheria na anatakiwa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

“Afisi ya DPP iliwateua watu 20 kati ya watu 2,031 waliomba nafasi za kazi katika sekta ya teknolojia (ICT), fedha na ununuzi wa bidhaa kutoka jamii moja na dini moja na kuwaacha Wakenya wengine kutoka dini tofauti,” anadai Ocharo kupitia kwa wakili Omari.

Mlalamishi huyo anasema katiba inakataa ubaguzi na kuajiriwa kwa watu kutoka jamii moja katika afisi ya umma.

Mahakama imeombwa ifutilie mbali mahojiano yaliyoorodheshwa kuendelea kati ya Aprili 25-29, 2022.

Ocharo ameomba mahakama ya ELRC itenge siku ya karibu kabla ya Aprili 25, 2022 kusikiliza na kuamua kesi hiyo.

“Jinsi mkuki ni mtamu kwa nguruwe lakini ni mchungu kwa binadamu ndivyo DPP anatakiwa kufahamu kwa vile wakati huu ndiye anayeathiriwa,” Bw Omari akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending