Connect with us

General News

Mwaura afungua moyo baada ya jaribio kumvua taji la useneta – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwaura afungua moyo baada ya jaribio kumvua taji la useneta – Taifa Leo

Mwaura afungua moyo baada ya jaribio kumvua taji la useneta

Na SAMMY WAWERU

SENETA maalum Bw Isaac Mwaura ameelezea kuhusu mahangaiko aliyopitia kufuatia jaribio la chama tawala cha Jubilee kumvua wadhifa wake mwaka uliopita.

Aliteuliwa kama seneta maalum 2017, kupitia Jubilee na amesema jaribio la kubanduliwa bungeni lilitokana na msimamo wake kuunga mkono Naibu wa Rais, William Ruto kuwania urais katika uchaguzi mkuu. “Mwaka uliopita wakati nilisema ya kwamba kiongozi anaweza kuwa wa chini awe rais, nilifunguliwa kesi saba na kufikishwa kortini zaidi ya mara thelathini,” Bw Mwaura akasema, akisimulia masaibu yaliyomfika.

Alisema hayo katika kikao na wahudumu wa tuktuk na maruti mtaa wa Githurai 45, ulioko eneobunge la Ruiru, Kiambu. Seneta huyo ni mwandani wa Bw Ruto, na anamezea mate kiti cha ubunge Ruiru kupitia UDA. Naibu rais ndiye kinara wa chama hicho, na anawania urais katika uchaguzi mkuu chini ya muungano wa Kenya Kwanza.

Uhusiano wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake ulianza kuingia doa baada ya kiongozi wa nchi na kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, kutangaza kuzika tofauti zao za kisiasa mnamo Machi 2018 kupitia salamu za maridhiano, maarufu kama Handisheki. Ni kutokana na maridhiano hayo, Ruto amekuwa akilalamikia wandani wake kuhangaishwa na serikali.

Novemba 2021, mahakama kuu iliharamisha kuondolewa kwa Bw Mwaura Jubilee ikikosoa kamati ya nidhamu chamani kwa kile ilitaja kama “kutozingatia sheria kumbandua”. Korti kwenye maelezo yake ilisema UDA ina mkataba wa makubaliano na mrengo tawala wa Jubilee.

Bw Isaac Mwaura, seneta maalum akizungumzia wahudumu wa tuktuk na Maruti Githurai 45, Ruiru, Kaunti ya Kiambu…Picha/ SAMMY WAWERU

“Nimeteuliwa kuwa bungeni mara mbili, lakini wadhifa wa kuteuliwa unaweza ukatolewa nyama mdomoni,” Mwaura akasema. “Liwalo na liwe, nitaendelea kutetea mahasla wenzagu (nembo ambayo Dkt Ruto hujitambua nayo),” akaelezea. Anawakilisha wananchi wenye ulemavu bunge la seneti. Aidha, aliteuliwa mara ya kwanza kuingia bunge la kitaifa 2013, kupitia chama cha ODM.

Maseneta wengine waliobanduliwa na Mwaura ni pamoja na; Millicent Omanga, Mary Seneta, Falhada Dekow, Naomi Waqo na marehemu Victor Prengei. Chaguzi za mchujo wa vyama zinazotarajiwa Aprili, Bw Mwaura atatoana kijasho na mbunge wa sasa Ruiru, Simon King’ara, katika UDA.

Aliyekuwa mbunge wa eneo hilo, Bi Esther Gathogo vilevile anamezea mate kiti hicho kupitia chama cha Jubilee.

Seneta maalum, Bw Isaac Mwaura akimpa mama leso yenye nembo yake kuwania ubunge Ruiru, baada ya kukutana na wahudumu wa tuktuk na Maruti Githurai…Picha/ SAMMY WAWERU

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending