Connect with us

General News

Mzazi aliyepinga CBC kortini ajiondoa, waziri Magoha sasa ataka kesi itupwe – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mzazi aliyepinga CBC kortini ajiondoa, waziri Magoha sasa ataka kesi itupwe – Taifa Leo

Mzazi aliyepinga CBC kortini ajiondoa, waziri Magoha sasa ataka kesi itupwe

NA RICHARD MUNGUTI

WAZIRI wa Elimu Prof George Magoha, Jumatatu aliomba majaji watatu wa Mahakama Kuu watupilie mbali kesi inayopinga mfumo mpya wa elimu (CBC), akisema mtaala huo umepiga hatua kubwa.

Kupitia kwa wakili Philip Murgor, Prof Magoha alipinga ombi la wakili Nelson Havi kuruhusiwa kuendelea na kesi baada ya mzazi Esther Ang’awa kuomba wamruhusu ajiondoe.

Bi Ang’awa alisema tangu awasilishe kesi hiyo ya kupinga CBC asasi mbalimbali za serikali zimekuwa zikimwandama.

“Sitaki kuendelea na kesi hii kwa vile naandamwa. Nahofia elimu ya mtoto wangu itaborongwa na washika dau endapo nitaendelea na kesi,” alisema Bi Ang’awa katika ombi kortini.

Akafafanua: “Haki zangu na za mtoto wangu zinakandamizwa. Nahofia elimu ya mtoto wangu itaborongwa na washika dau endapo nitaendelea na kesi hii,” akasema Bi Ang’awa katika ombi alilowasilisha mahakamani.

Katika kesi aliyoshtaki Waziri wa Elimu Prof Magoha, Waziri wa Usalama Dkt Fred Matiang’í, taasisi ya kukuza mitaala (KICD), chama cha kitaifa cha kutetea haki za walimu (KNUT), Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na vyama vya wakuu wa shule za msingi (Kepsha) na Kuppet, Bi Ang’awa alisema mfumo wa CBC ni ghali na unawalimbikizia mzigo mzito wanafunzi na wazazi.

Kufuatia dhulumu anayopata pamoja na mwanawe, Bi Ang’awa ameomba akubaliwe kuondoa kesi hiyo.

Akiwasilisha ombi la kuruhusiwa aendelee na kesi hiyo Bw Havi alisema kesi hiyo inaathiri mamilioni ya wanafunzi kote nchini.

“Kesi hii iko na umuhimu wa kitaifa kutokana na athari zake. Naomba nikubaliwe kuendelea nayo kama wakili niliyeelezwa athari za mtaala huu mpya unaokandamiza haki za mamilioni ya wanafunzi,” alisema Bw Havi.

Bw Havi alisema alipoapishwa kuwa wakili aliapa kutetea na kutenda haki kwa wote.

“Kesi hii inazua masuala mazito ya kikatiba. Uamuzi wa kesi hii utazingatia haki za kimsingi za wanafunzi,” alisema Bw Havi akiomba akubaliwe kuendeleza kesi hiyo.

Lakini mawakili wanaotetea taasisi mbali mbali walipinga ombi la Bw Havi wakisema “hana uhusiano wowote na mlalamishi.”

Majaji hao walitenga Juni 9, 2022 kuamua ikiwa ama watamruhusu Bw Havi kuendelea na kesi hiyo au wataifutilia mbali.

 

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending