Mahakama ya Garissa imemzuilia zaidi naibu wa chifu kutoka Wajir aliyeshtakiwa kwa ubakaji hadi pale ambapo mashahidi wote watatoa ushuhuda wao.
Amri hiyo ilitolewa baada ya afisi ya Mkuregenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kuwasilisha ombi la kutaka mshukiwa, Kalmoi Shale Ahmed kusalia kizuizini kwa muda.
Aliiomba mahakama imuwachilie kwa dhamana lakini afisi ya DPP ilikataa na kusema huenda angetatiza uchunguzi na hata kuwatishia mashahidi akitumia mamlaka yake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.