– Ripoti zinaonyesha kuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi walivamia bohari hilo Ijumaa, Aprili 30 alasiri
– Mmiliki mwenye bohari hiyo ambaye ana leseni ya bastola alionekana akiwafyatulia risasi majangili hao ila alikosa na risasi hiyo ikampata mlinzi huyo kichwani, na kumuua papo hapo
-Wakati wa tukio hilo, raia mwingine ambaye alikuwa akipita alipigwa risasi kimakosa na baadaye alikimbizwa hospitalini
Polisi jijini Nairobi wanachunguza kisa ambapo mtu asiyejulikana alimpiga risasi bawabu aliyekuwa akilinda bohari moja Moi Avenue.
Ripoti zinaonyesha kuwa watu wanaoshukiwa kuwa majambazi walivamia bohari hilo Ijumaa, Aprili 30 alasiri.
Mmiliki mwenye bohari hiyo ambaye ana leseni ya bastola alionekana akiwafyatulia risasi majangili hao ila alikosa na risasi hiyo ikampata mlinzi huyo kichwani, na kumuua papo hapo.
Umati wa watu ulikusanyika eneo la tukio huku kila mmoja akitaka kujua kilichokuwa kimetokea
Kulingana na ripoti ya polisi, washukiwa hao wawili walikuwa miongoni mwa genge la majangili watatu ambao walimshambulia na kumpora mtu asiyejulikana wakiwa wamejihami kwa bastola.
Ripoti hiyo ilisema maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria waliwaamuru wajisalimishe, lakini badala yake walianza kuwafyatulia risasi.