Connect with us

General News

Najuta kujiunga na Ford-Kenya, Wangamati sasa aungama – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Najuta kujiunga na Ford-Kenya, Wangamati sasa aungama – Taifa Leo

Najuta kujiunga na Ford-Kenya, Wangamati sasa aungama

NA BRIAN OJAMAA

GAVANA wa Bungoma, Wycliffe Wangamati ameeleza majuto ya kujiunga na chama cha Ford Kenya.

Wangamati alisema chama hicho kilichomfadhili akashinda ugavana, kimehujumu utawala wake wa miaka mitano.

Bw Wangamati aliyehama chama hicho Ijumaa na kujiunga na Democratic Action Party (DAP), alisema hakuwahi kutulia katika chama hicho tangu alipoingia ofisini.

Akizungumza akiwa eneobunge la Tongaren mnamo Jumamosi, Gavana

Wangamati alisema chama hicho kimekuwa kizingiti katika utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo.

Alisema ndiye gavana wa pekee nchini ambaye ameshtakiwa mara kadhaa kwa kuanzisha miradi ya maendeleo katika kaunti yake.

“Nilipoajiri wasimamizi wa vijiji, ni chama changu cha zamani kilichoenda kortini kusimamisha mpango huo,” alisema gavana huyo.

Pia alidai kuwa chama hicho kilifadhili mswada wa kumuondoa ofisini la – kini akaokolewa na madiwani.