Connect with us

General News

NCIC yashtakiwa kuhusu marufuku ya ‘Sipangwingwi’ na ‘Watajua hawajui’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

NCIC yashtakiwa kuhusu marufuku ya ‘Sipangwingwi’ na ‘Watajua hawajui’ – Taifa Leo

NCIC yashtakiwa kuhusu marufuku ya ‘Sipangwingwi’ na ‘Watajua hawajui’

NA RICHARD MUNGUTI

VUGUVUGU la mawaki – li limewasilisha kesi katika mahakama kuu kupinga marafuku ya matumizi ya maneno “hatupangwingwi” na “watajua hawajui”.

Kupitia kwa mawakili Felix Kiprono na Vincent Yegon, Chama cha Mawakili Limited (CML) kinaomba mahakama kuu ifutilie mbali marufuku iliyotolewa na Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) dhidi ya matumizi ya maneno hayo.

Maneno haya yamo katika wimbo uliotungwa na mwanamuziki Tonny Kinyanjui almaarufu Exray anayemshikirisha Naibu wa Rais William Ruto.

Katika wimbo huo, Dkt Ruto ananukuliwa akisema “kama vile Wakenya wanasema hawapangwingwi hata mimi kama hasla ninasema sipangwingwi”.

Mawakili Kiprono na Yegon wameeleza katika kesi waliyoshtaki kwamba maneno hayo hayashirii chuki ama uchochezi.

Chama hiki cha mawakili kimedai NCIC inatumia mamlaka yake vibaya kukandamiza haki za wananchi kufurahia uhuru wa usemi.

CML inaomba mahakama kuu itumie mamlaka yake kutafsiri maneno haya yaliyotangazwa na NCIC mnamo Aprili 8,2022 kuwa ya uchochezi na kueneza hisia za kikabila.

Wanaomba mahakama kuu izuie NCIC kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa ama wanamuziki ambao watayatumia.

“Tume ya NCIC imejiingiza katika ulingo wa siasa na kuacha majukumu iliyobuniwa kutekeleza,” Bw Kiprono akasema katika ushahidi aliowasilisha mahakamani.