– Safari ya Joho na Junet kumuona Baba Dubai ilikuwa ya kifahari ndani ya ndege ambayo hutoza mamilioni
– Kuna madai kuwa safari hiyo ilitumia fedha za mlipa ushuru kutoka bajeti ya Ikulu
– Kwa saa moja ndege hiyo hutoza KSh1.3M bila vinywaji au vyakula vya wateja walioabiri
Gavana wa Mombasa Hassan Joho na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed waliwasili Dubai kumuona kinara wa ODM Raila Odinga baada ya kufanyiwa upasuaji.
Wawili hao waliondoka Mombasa Alhamisi, Julai 9 wakiabiri ndege la kifahari ambalo hugharimu takriban KSh 1.3M kwa kila saa.