[ad_1]
Ngirici kuwania ugavana kama mwaniaji huru
NA GEORGE MUNENE
MBUNGE Mwakilishi wa Kike wa Kirinyaga Wangui Ngirici, amesema kwamba atawania ugavana wa kaunti kama mwaniaji wa kujitegemea.
Akiongea Jumanne kwenye mkutano wa kampeni katika eneo la Karumandi eneobunge la Gichugu, Bi Ngirici alisema amechoshwa na vyama vya kisiasa.
Alielezea jinsi alivyodhulumiwa na chama cha United Democratic Alliance (UDA) baada ya kuwekeza rasilimali zake na muda mwingi katika chama hicho.
Bi Ngirici alielezea imani kwamba wakazi wa Kirinyaga watampigia kura kiongozi mchapa kazi lakini sio vyama vya kisiasa.
“Nimeamua kuwania kiti hicho bila tiketi ya chama chochote kwa sababu ninafahamu kuwa wakazi hupigia kura watu binafsi lakini sio vyama au mirengo ya kisiasa,” akaeleza.
[ad_2]
Source link