Connect with us

General News

Ni wakati mwafaka wa kudhibiti kinywa kichafu cha Moses Kuria – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ni wakati mwafaka wa kudhibiti kinywa kichafu cha Moses Kuria – Taifa Leo

WANDERI KAMAU: Ni wakati mwafaka wa kudhibiti kinywa kichafu cha Moses Kuria

NA WANDERI KAMAU

UKAMILIFU wa jamii mbalimbali duniani husheheni uwepo wa tamaduni tofauti baina yao.

Duniani kote, hakuna jamii ambayo haina utamaduni wake maalum.Hata hivyo, jamii husika huwa haijichagulii utamaduni ambao itafuata ama kuzingatia, bali huendeleza tamaduni hizo kulingana na msingi uliowekwa na mababu zake.

Tamaduni hizi zilitoka kwa mababu zetu karne nyingi zilizopita.Utamaduni wowote huwa ni utambulisho wa jamii husika. Zaidi ya hayo, hakuna utamaduni i bora kuliko mwingine.

Licha ya ufahamu huu, inasikitisha kuwa baadhi ya wanasiasa nchini wameamua kutoa matamshi ya kuzigonganisha jamii kwa misingi ya tofauti za tamaduni zao.

Mfano bora wa wanasiasa hao ni mbunge Moses Kuria wa Gatundu Kusini.

Kwenye msururu wa mikutano ya kisiasa ambayo Naibu Rais William Ruto alifanya katika eneo hilo Ijumaa, Bw Kuria alitoa matamshi ambayo hayawezi kutamkika wala kuandikika dhidi ya jamii moja nchini.

Cha kushangaza ni kwamba, hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo kutoa matamshi kama hayo.

Mnamo 2015, Bw Kuria alishtakiwa kwa kutoa matamshi yaliyoilenga na kuisawiri vibaya jamii ya Waluo.

Kinaya ni kuwa, kesi hiyo ilimalizika baadaye katika hali tatanishi.

Bw Kuria pia amekabiliwa na kesi nyingine ya uchochezi, ambapo alitishia kutoa silaha kwa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) katika eneo lake ili “kujilinda.”

Maswali yanayoibuka ni: Mbona kesi zinazomkabili mbunge huyo huwa zinafutiliwa mbali ama kukamilika katika hali tatanishi licha ya ushahidi wa wazi kuwepo?

Je, yeye ni mwanasiasa ‘spesheli’ ambaye yuko huru kusema lolote alitakalo bila kuogopa lolote?

Kuna mkono fiche unaomlinda Bw Kuria dhidi ya kukabiliwa vikali na sheria?

Umefika wakati mwanasiasa huyo kukabiliwa vikali ili kuwa mfano kwa wanasiasa wengine wanaolenga kuanza kutumia mbinu hii chafu kufufua upya uhasama na chuki za kikabila.

Matamshi ya Bw Kuria wakati mwingine huzua tashwishi kuhusu urazini wake kama mwanadamu.

Kwenye Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) wa chama cha UDA, chake Dkt Ruto katika Uwanja wa Michezo wa Kasarani, Jumatano, jijini Nairobi, Bw Kuria alidai alishirikiana na wanasiasa wengine kumwibia – kwa faida yake – kura Rais Uhuru Kenyatta kwenye chaguzi za 2013 na 2017.

Bila kuogopa, Bw Kuria hata aliwataja wanasiasa aliodai walishirikiana naye kutekeleza maovu hayo. Ni lini mdomo wake utazimwa ili kuwahakikishia usalama Wakenya?

[email protected]

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending