[ad_1]
Mwanasheria Mkuu (AG) wa kwanza wa Kenya baada ya uhuru wa nchi hiyo, Sir Charles Njonjo amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 101.
Akitangaza msiba huo, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Sir Njonjo ambaye ni maarufu nchini Kenya amefariki leo asubuhi Jumapili ya Januari 2, 2022.
Rais Kenyatta amesema “Kifo cha Mheshimiwa Njonjo siyo pigo tu kwa familia yake, marafiki na jamaa zake, bali ni pigo kwa Wakenya wote, Bara la Afrika kwa sababu ya juhudi zake za kujenga msingi wa kupatikana uhuru wa Wakenya,”.
Njonjo anayechukuliwa na wengi ni mtu mwenye nguvu baada ya Moi, wakati wa kuvunjika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mwaka 1977, alikuwa ni mmoja wa watu waliofurahia.
Pia, alitaka Jumuiya ya Afrika Mashariki ife na alifanya juhudi kuiua na ilipokufa Juni 1977, ilielezwa alikwenda kwenye hoteli ya Norfolk jijini Nairobi na kununua chupa tano za ‘champagne’ kusherehekea kifo cha EAC.
Sir Njonjo ni mjumbe pekee katika baraza la kwanza la mawaziri lililoundwa na Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta mwaka 1963 ambaye mpaka sasa alikuwa hai.
[ad_2]
Source link