[ad_1]
ODM yajiandaa kumnadi Nassir kutwaa ugavana
NA WINNIE ATIENO
VIONGOZI wa chama cha ODM tawi la Mombasa wameanza kuweka mikakati upya kumpigia debe mwaniaji wao wa ugavana, Bw Abdulswamad Nassir.
Wakuu wa chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao, Bw Mohammed Khamis, jana walikongamana katika afisi ya Gavana Hassan Joho kujadiliana kuhusu watakavyoendesha zoezi hilo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na makundi ya vijana ambao watategemewa kupanga kampeni hadi mashinani.
“Tunataka kuhakikisha umoja wetu unadumishwa na kwamba viongozi wote wa ODM wanapigiwa kura ya suti,” akasema mmoja wa waliohudhuria mkutano huo, Bw Hamza Kombo.
Kiongozi wa vijana Bw Stewart Ndolo alisema watahakikisha kwamba Bw Nassir anashinda uchaguzi wa ugavana.
Bw Nassir anashindania kiti hicho dhidi ya aliyekuwa gavana wa Nairobi, Bw Mike Sonko wa Chama cha Wiper, aliyekuwa seneta wa Mombasa, Bw Hassan Omar (UDA), na Naibu Gavana, Dkt William Kingi (PAA).
Next article
ANC yafufua wito Mudavadi awe naibu wa Ruto
[ad_2]
Source link