Connect with us

General News

PAA yakoroga urithi wa Gavana Joho Mombasa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

PAA yakoroga urithi wa Gavana Joho Mombasa – Taifa Leo

PAA yakoroga urithi wa Gavana Joho Mombasa

WINNIE ATIENO NA ANTHONY KITIMO

KINYANG’ANYIRO cha kurithi kiti cha Gavana wa Mombasa, Bw Hassan Joho, kimechukua mkondo mpya baada ya kuibuka kuwa, chama cha Pamoja African Alliance (PAA) kimeanza kucheza karata za chini kwa chini.

Wakati uo huo, chama cha Jubilee kimethibitisha kwamba hakitakuwa na mgombea wa ugavana Mombasa, bali kitaunga mkono ODM chini ya Muungano wa Azimio la Umoja.

Imebainika kuwa maafisa wakuu wa chama cha PAA chake Gavana Amason Kingi wa Kilifi, walikutana wikendi na Mbunge wa Kisauni, Bw Ali Mbogo, pamoja na Naibu Gavana wa Mombasa, Dkt William Kingi, ambao wanamezea mate kiti hicho.

Baada ya mkutano huo, wawili hao wameanza kufanya kampeni za pamoja za ugavana.

Bw Mbogo, ambaye ni mwanachama wa Wiper, alisema lengo lao ni kuzuia mgawanyiko wa kura za jamii ya Wamijikenda katika kinyang’anyiro cha ugavana.

“Mimi na Dkt Kingi tumesema kila mtu atafanya siasa yake, lakini itafika mahali lazima tutatembea barabara moja. Jukumu letu ni kuleta jamii zetu pamoja. Wapinzani wetu watajiuliza maswali mengi sababu ya ushirikiano wetu,” akasema Bw Mbogo.

Dkt Kingi ni mmoja wa wanasiasa wanaotaka kushindania tiketi ya chama cha ODM ya ugavana.

Hata hivyo, dalili kufikia sasa zimeashiria ushindani mkubwa katikla kivumbi kizima ni kati ya Mbunge wa Mvita, Bw Abdulswamad Nassir, na mfanyabiashara, Bw Suleiman Shahbal, ambao pia wanataka tiketi ya ODM.

Aliyekuwa Seneta Hassan Omar anatazamiwa kuwania usimamizi wa kaunti hiyo kuu ya Pwani kupitia United Democratic Alliance (UDA).

Katika chaguzi zilizopita, Bw Joho aliteua manaibu wake kutoka kwa jamii ya Wamijikenda ili kusawazisha uwakilishi wa jamii kuu za asili ya Pwani kwenye utawala wake.

Naibu wake wa kwanza alikuwa Bi Hazel Katana, ambaye alihudumu hadi mwaka wa 2017.

Kisha Dkt Kingi akapewa nafasi hiyo katika kipindi cha pili cha uongozi wa Bw Joho.

Bw Mbogo, ambaye anategemea pakubwa kura za Kisauni katika azimio lake, alisema hatatosheka na nafasi ya unaibu gavana mwezi Agosti.

“Ukiona kobe ameinama, jua sheria inatungwa. Wanatudanganya na unaibu gavana; eti wao wachukue ugavana sisi tusalie nambari mbili.

“Safari hii hatutaki nambari mbili, twataka ugavana,” alisisitiza Bw Mbogo.

Naye Dkt Kingi alisema kwa sasa wote wataendelea kushindania tiketi ya kugombea ugavana, na yule atakayeshindwa atamuunga mkono mwenzake.

Chama cha ODM kimekuwa kikiendeleza utafiti wa kura ya maoni kubainisha mgombeaji aliye na umaarufu zaidi kati ya watatu wanaotaka tiketi yaake ya chungwa, kabla kuamua iwapo kutakuwa na haja ya kura ya mchujo Mombasa.

“Akishinda nitamuunga mkono, nikishinda ataniunga ili tufanye kazi pamoja. Huo ndio undugu ambao utastawisha Mombasa,” akaeleza.

Uamuzi wa chama cha Jubilee kutosimamisha mgombeaji wa ugavana katika kivumbi cha Mombasa kumepiga jeki ODM.

Hata hivyo, vyama vingine tanzu vya vuguvugu la Azimio la Umoja, kama vile PAA na Wiper, bado vinaonekana kutaka kuwa na wagombeaji.

Ni hali hii huenda ikagawanya kura za wafuasi wa kinara wa ODM, Bw Raila Odinga, katika ushindani wa kiti cha ugavana.

Aliyekuwa Naibu Gavana Bi Katana, ambaye ndiye mwenyekiti wa Jubilee mjini Mombasa, alisema mashauriano yanaendelea kuhusu jinsi Azimio itakavyogawa viti vya kisiasa, lakini akathibitisha chama hicho tawala hakina mgombeaji ugavana Mombasa.

“Tunatarajia ODM na vyama vingine tanzu kurejesha mkono kwa Jubilee katika nafasi nyingine ambazo tutakuwa na wagombeaji. Mashauriano yanaendelea,” akasema.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending