Connect with us

General News

Pasta ashtakiwa kwa ulaghai wa mafuta ya utakaso – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Pasta ashtakiwa kwa ulaghai wa mafuta ya utakaso – Taifa Leo

Pasta ashtakiwa kwa ulaghai wa mafuta ya utakaso

NA RICHARD MUNGUTI

PASTA aliyepokea Sh730,000 kutoka kwa Askofu wa Kanisa waliyehudumu pamoja akidai atamnunulia mafuta ya utakaso kutoka ng’ambo mwaka 2022 ameshtakiwa kwa ulaghai.

Hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani jijini Nairobi Bi Wendy Kagendo alifahamishwa badala ya Pasta Martin Muraya Sammy kuendelea kuhudumu pamoja na Askofu Samuel Mburu Kerige, alihama na kufungua kanisa lake katika eneo la Thika, kaunti ya Kiambu.

“Mshtakiwa ni Pasta aliyekuwa akihudumu kwa kanisa moja na mlalamishi ambaye ni Askofu makosa haya yalipotendeka mnamo Novemba 2020,” Bi Kagendo alielezwa na wakili aliyemwakilisha Muraya.

Muraya alikabiliwa na shtaka la kupokea Sh730,000 kati ya Novemba 9-12, 2020 kwa njia ya udanganyifu.

Shtaka lilisema Muraya alipokea pesa hizo akidai alikuwa na uwezo wa kumnunulia Askofu Kerige mafuta maalum ya upako.

Kiwango cha mafuta ambayo Muraya angelimnunulia kiongozi wake wa kiroho hakikusemwa ila yalikuwa ya thamani ya Sh730,000.

Muraya alikana shtaka kisha wakili akaomba aachiliwe kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu.

“Mshtakiwa ni Pasta na mlalamishi ni Askofu. Wote wawili ni watumishi wa Mungu. Naomba hii mahakama imwachilie kwa dhamana isiyo ya kiwango cha juu,” hakimu alielezwa.

Wakili huyo alieleza mahakama, “Mshtakiwa hana mapato kwa vile hata alishindwa kujilipia dhamana atoke korokoro ya polisi tangu akamatwe Aprili 30, 2022.”

Hakimu alimwuliza mshtakiwa kanisa yao na kule walipokuwa wanahudumu.

Mshtakiwa alinyamaza kimya kiasi kisha akasema, “Nilihamishia huduma yangu Thika kutoka Nairobi. Hatuko pamoja na mlalamishi.”

Bi Kagendo alimwuliza mshtakiwa iwapo pia alikuwa anajaribu kutumia ujanja kupewa kiwango cha dhamana kisicho cha juu kwa kudai “wanahudumu pamoja na mlalamishi.”

Mshtakiwa alisisitiza wanashirikiana pamoja na mlalamishi katika mahubiri ya mikutano ya hadhara.

Hakimu alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh500,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.

Endapo Pasta huyo atakosa dhamana hiyo pia hakimu alimpa dhamana ya pesa taslimu Sh300,000.

Hakimu aliamuru kiongozi wa mashtaka Bi Nancy Kerubo amkabidhi mshtakiwa nakala za mashahidi na kutenga Mei 18, 2022 siku ya kuteua siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Mshtakiwa alitiwa pingu na kupelekwa seli za mahakama ya Milimani.

Na wakati huo huo mwekezaji kutoka Sudan Kusini alishtakiwa kwa kushindwa kulipa deni la Sh359,261 kwa hoteli ya Nairobi Serena alipolala mle kwa siku 17.

Amir Ahmed Mohamed alikana alipokea deni hilo alipokodisha chumba cha kulala kati ya Aprili 12-28, 2022.

Bi Kagendo aliamuru Amir azuiliwe kituo cha Polisi cha Central hadi wakati wa yeye kulipia deni hilo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending