– Kifo cha Lugaliki kilithibitishwa na KMPDU mnamo Ijumaa, Julai 10
– Matabibu wenzake walimtaja kama daktari aliyekuwa na bidii kazini
– Mnamo Ijumaa, Julai 8, Waziri Kagwe alifichua kuwa takriban maafisa 257 wa afya wameambukizwa COVID-19 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini Ijumaa, Machi 13
Idara ya matabibu ilimpoteza mmoja wa madaktari stadi aliyekuwa mstari wa mbele katika kupambana na virusi hatari vya COVID-19.
Maisha ya Dkt Doreen yalikatizwa ghafla Ijumaa, Julai 10.
Dkt Lugaliki alipoteza maisha yake akiwa kazini akiwahudumia wagonjwa wa COVID-19. Picha: Adisa Lugaliki. Source: UGC
Muungamo wa Matabibu, Wanafamasia na madaktari wa meno (KMPDU) ulimtaja marehemu afisa huyo kama mwenye bidii sana kazini.
“Tumempoteza mtaalamu wa afya ya kike, mama, rafiki na mfanyikazi mwenzetu kutokana na makali ya COVID-19. Rambi rambi zetu kwa ndugu, jamaa na marafiki za Dkt Doreen Lugaliki,” KMPDU ilisema kwenye taarifa yake.
Hizi hapa ni baadhi ya picha zilizoashiria alikuwa dada mchangamfu:
Dkt Lugaliki alikuwa mtaalamu wa afya ya kike. Picha: Picha: Adisa Lugaliki. Source: Facebook
Daktari huyo alikuwa mmoja wa matabibu waliokuwa mtari wa mbele kupambana na COVID-19.
Lugaliki alikuwa daktari ambaye alihudumu kaunti ya Nairobi. Picha: Adisa Lugaliki. Source: Facebook
Lugaliki aliaga dunia akiwahudumia wagonjwa
Dkt Lugaliki aliaga dunia akipokea matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Source: Facebook
Luagliki alikuwa mama aliyejaa upendo na aliitembeza familia yake sehemu mbali mbali kujivinjari.
Ni bayana Doreen alimuenzi sana bintiye Picha: Adisa Lugaliki. Source: Facebook
Wenzake walimtaja kazini kama daktari aliyejitolea katika kazi yake.
Doreen Lugaliki kwenye ziara ya nchini Misri mnamo 2017. Picha: Adisa Lugaliki Source: Facebook
Madaktari wenzake waliomboleza kifo chake na hata kutuma rambirambi zao kwa familia ya marehemu.
Mnamo Ijumaa, Julai 8, Waziri Kagwe alifichua kuwa takriban maafisa 257 wa afya wameambukizwa COVID-19 tangu kisa cha kwanza kuripotiwa nchini Ijumaa, Machi 13.
Ugonjwa huo uliathiri zaidi ya Wakenya 8,900 kufikia Alhamisi, Julai 9 huku idadi ya vifo ikigonga.