1. Japo wengi wanatarajia kuwa anamtegemea baba yake Mike Sonko kujikimu, mrembo huyo amethibitisha kuwa anaweza kujisimamia. Huwa anaweka bidii ya mchwa kukimu familia yake changa.
Saumu alimkaribisha mwanawe wa pili Machi 2019. Picha: Saumu Mbuvi. Source: Instagram
2. Miezi kadhaa baada ya kujaliwa mtoto wa pili, bado anapendeza na kushikilia umbo lake ambalo hutamaniwa na wengi.
Saumu amekuwa akichumbiana na Seneta wa Lamu, Anwar Loitiptip. Picha: Saumu Mbuvi. Source: Instagram
3. Wiki chache zilizopita alitangaza kuwa anatazamia kufanya harusi na mpenzi wake na atatoa tarehe rasmi ya hafla hiyo
Saumu Mbuvi anajivunia kuwa mama ya mabinti wawili. Picha: Saumu Mbuvi. Source: Instagram
4. Mtindo wake mpya umewafurahisha wengi mtandaoni. Anaonekana kubadilisha mtindo wake wa mavazi na kuanza kuvalia mavazi rasmi.
Saumu Mbuvi amekuwa akitesa na mtindo wake mpya wa mavazi. Picha:Saumu Mbuvi. Source: Instagram
5. Saumu amekuwa kwenye mstari wa mbele kupigania haki ya wanawake ambao wamekuwa katika uhusiano mbaya. Mrembo huyo amekuwa akiwaomba wanawake kuondoka katika mahusiano mabaya.