Wafungwa 20 katika vituo vya polisi vya Thika na Makongeni wamepatwa na virusi vya maradhi ya Covid-19.
Kamanda wa polisi kaunti ya Kiambu Ali Nuno alisema visa hivyo ni 17 kutoka Makongeni na vitatu kutoka Thika.
Habari Nyingine: Jumatatu Julai 20: Papa Shirandula kuzikwa kesho kijijini Namisi
Wafungwa 17 katika kituo cha polisi cha Makongeni walipatwa na coronavirus. Picha: K24
Source: UGC
Kulingana na ripoti ya Citizen, 20 hao walipatikana kutoka kwa sampuli 68 zilizokuwa zimechukuliwa.
Ukaguzi huo ulianza baada ya wafungwa wawili kuonyesha dalili za kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.
Habari Nyingine: Trans Nzoia: Mume amfurusha mke wake na kuanza kuishi na mpenziwe wa kiume
Wafungwa wengine 3 katika kituo cha polisi cha Thika walipatwa na Copvid-19.
Source: UGC
Aidha inaarifiwa kuwa tayari maafisa kadhaa wa polisi walifanyiwa ukaguzi pia na sasa wanasubiri matokeo.
Ripoti zinasema tayari kuna maafisa sita katika kaunti hiyo ambao wamekwisha kutwa na virusi hivyo tangu ugonjwa huo uzuke mwezi Machi.
Habari Nyingine: : Marafiki wa DP Ruto wageukia maombi baada ya masaibu kuwazidi siasani
Serikali iliwaachilia wafungwa wa makosa madogo ili kupunguza mtagusano gerezani.
Source: Twitter
Serikali mapema Aprili iliwaachilia huru wafungwa wa makosa madogo kama njia moja ya kupunguza msongamano kwenye magereza.
Virusi vya Covid-19 huambukizwa kwa haraka baina ya maeneo yenye mtagusano mkubwa wa watu.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videos