Connect with us

General News

Profesa Magoha asinyamaze walimu wakuu wakiwaongezea wazazi gharama zaidi

Published

on

Profesa Magoha asinyamaze walimu wakuu wakiwaongezea wazazi gharama zaidi

WAZAZI wengi wanalalamikia hatua ya walimu wakuu wa shule za upili kuwataka wawanunulie watoto wao, wanaojiunga na kidato cha kwanza, vitu vingi “visivyo na umuhimu mkubwa”.Baadhi ya shule zimeagiza kwamba wanafunzi hao wanunuliwe vitu kama vile vifaa vya michezo, jembe, panga, karatasi za kutoa chapa, miongoni mwa vingine ambavyo sio vya kimsingi.

Hii ni kinyume na agizo ambalo Waziri wa Elimu George Magoha alitoa mnamo Aprili 11 katika Taasisi ya Kuandaa Mitaala Nchini (KICD), Nairobi, alipozindua rasmi shughuli ya uteuzi wa wanafunzi wa kujiunga na kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo wa 2022.

Profesa Magoha asinyamaze kana kwamba amesahau kwamba aliwaagiza walimu wakuu kutowaongezea wazazi gharama zaidi wakati huu ambapo wengi wao wanazongwa na makali ya kuzorota kwa uchumi.

Aidha, waziri huyu akumbuke kuwa mwenendo huu wa walimu wakuu, haswa wa shule za upili za mabweni, kuwataka wazazi wawanulie vitu vingi huenda ukachangia baadhi yao kushindwa kumudu gharama hiyo.

Matokeo yake ni kwamba watoto wengi watakosa kujiunga na shule za upili, hali inayoenda kinyume na sera ya serikali ya kuhakikisha kuwa watoto wote waliofanya mtihani wa KCPE wanawezeshwa kuendelea na masomo.

Comments

comments

Trending