Wabunge 65 kati ya 97 wa kike walipiga kura na kumuondoa Ngirici kama mweyekiti wa KEWOPA. Picha: Purity Ngirici. Source: Facebook
Mnamo Jumanne, Julai 7, wabunge 65 kati ya 97 walipiga kura kumuondoa Ngirici kama mwenyekiti wa kamati hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kiambu Gathoni wa Muchomba.
Wabunge wa KEWOPA walimshtumu Ngirici kwa uongozi duni katika chama hicho kando na kushindwa kulinda masilahi ya wanawake katika uongozi.
Naibu wake atakuwa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kisumu Roza Buyu akisaidiwa na seneta mteule Millicent Omanga.
Katibu Mkuu wa chama hicho atakuwa mbunge Mishi Mboko akisaidiwa na Charity Chepkwony.
kwa upande wake, mwanasiasa huyo alisema hatua hiyo haikutekelzwa kwa njia halali.
“Ningependa kusema kwamba mkutano uliyofanyika haukua halali na haukufuata utaratibu kulingana na katiba ya KEWOPA,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Ngirici amekuwa mkosoaji mkuu wa Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru.
Aliunga mkono mpango wa wajumbe kumng’atua gavana huyo mamlakani huku mumewe pia akiupigia upato.
Mnamo Juni 13, Andrew Ngirici alihojiwa kwa saa mbili na maafisa wa kituo cha Mwea Mashariki.
Alikuwa ametishia kuandaa maandamano iwapo seneti itafanya maamuzi ya kuandaa kamati ya wawakilishi 11 kumpiga msasa Waiguru na kusikiza malalamishi dhidi yake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.