– Familia ya Raila Odinga imekiri kuwa kinara huyo wa chama cha ODM yuko katika hospitali nchini Dubai
– Oburu Odinga alisema Raila alisafiri ili kufanyiwa upasuaji ambao alisema hauna tishio lolote kwa afya yake
– Mtandao wa Twitter ulilipuka huku Wakenya wakimtakia Baba nafuu ya haraka
Kinara wa ODM Raila Odinga yuko nchini Dubai ambapo nduguye Oburu Odinga amesema alienda kufanyiwa upasuaji.
Familia ya Raila ilifichua hayo baada ya siku kadhaa za mjadala mtandaoni kuhusu hali ya afya ya kigogo huyo wa kisiasa.

Kinara wa ODM Raila Odinga. Raila yuko nchini Dubai kupokea matibabu.
“Jakom (Raila) yuko nje ya nchi kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mgongo. Si suala kubwa la kiafya. Kwa hivyo yuko sawa,” Oburu aliambia gazeti la Nation.
Familia yake ilisema yuko katika hospitali moja ya Ujerumani nchini Dubai ambapo atapata matibabu hayo.

Kinara wa ODM Raila Odinga inaarifiwa anapokea matibabu Dubai.
Mwanablogu Dennis Itumbi ndiye alikuwa wa kwanza kuzua maswali kuhusu hali ya kiafya ya Raila kupitia mtandao.
Baadaye mwelekezi wa mawasiliano ndani ya chama cha ODM Philip Etale alipuuza habari kuwa Baba amesafiri kutafuta matibabu.
Wakenya Alhamisi walifurika kwenye mtandao kumtakia Baba nafuu ya haraka