Katibu katika wizara ya barabara, ujenzi na miundo misingi nchini Charles Hinga alipozuru Elburgon kaunti ya Nakuru kuzindua mradi wa Kazi Mtaani. Picha: Bernard Waweru Source: Facebook
Mazungumzo yao yaliendelea vizuri huku Rais akiskika kufurahia mazungumzo hayo na kuwapa kicheko
“Habari ya Elburgon? Rais alisema huku Wanjiru akizidi kumpa heko kwa kuwapa kazi.
Kwa wakati mmoja, wawili hao walianza kuzungumza kwa lugha ya mama ya Kikuyu huku binti huyo akimuomba Rais waonane.
Aidha Rais alisema vijana wanaofaidika na mradi huo watakuwa wakifanya kazi kwa siku 11 ili wengine pia wapate nafasi hiyo.
“Si kukataa, lakini tunataka tufikie vijana wengi iwezekanavyo. Wewe Shiro ufanye 11 na kisha mwingine, tena wewe urudi zingine 11 hivyo hivyo,” alisema Rais.
Aidha aliahidi kupanga kukutana na msichana huyo atakapotembea eneo la Elburgon.
“Haya wacha tutaona, nitakuja kuwatembelea,” Uhuru alimwambia msichana huyo baada ya kusema ana
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.