Rais mpya wa Malawi Lazarus Chakwera amewarai wananchi kutoka dini mbali mbali kutangamana pamoja ili kuombea nchi kwa ajili ya janga la ugonjwa wa corona
Chakwera alisema nchi hiyo inapaswa kufunga na kuomba mfululizo kwa siku tatu ili kukemea ugonjwa huo ambao umeangamiza mamilioni ya watu ulimwenguni.
Nchi hiyo itaanza maombi maalum Alhamisi, Julai 16 na yatakamilika Jumamosi, Jula 18 ikifuatiwa na mkutano wa shukuran Jumapili, Julai 19.
” Rais amewataka wananchi wote kutoka dini mbali mbali watangamane kwa siku 3 ili wafunge na kuomba kwa ajili ya janga la corona, pia Rais amewataka wananchi wajumuike katika mkutano wa shukran ambao unatarajiwa kufanyika Jumapili, Julai 18,” Taarifa kutoka kwa afisi ya rais ilisoma.