Connect with us

General News

Rais kukutana na wanabodaboda – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Rais kukutana na wanabodaboda – Taifa Leo

Rais kukutana na wanabodaboda

Na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta ameitetea serikali yake dhidi ya madai ya naibu wake, William Ruto, kwamba inawadhulumu wahudumu wa bodaboda.

Akiwahutubia wananchi katika mtaa wa Kariobangi, Nairobi, Ijumaa, kiongozi wa taifa alisema madai hayo hayana msingi wowote na kwamba Ruto anatumia wahudumu wa bodaboda kuendesha siasa za kujitakia makuu.

“Mumedanganywa kwamba serikali haiwataki wanabodaboda. Hiyo sio kweli, hatuna shida na biashara za kihalali. Kile tunasisitiza ni kwamba lazima sheria ifuatwe na mambo yaendeshwe kwa mpango,” Rais Kenyatta akasema baada ya kufungua rasmi Hospitali ya Watoto ya Mama Margaret Kenyatta katika mtaa wa Kariobangi North.

Rais Kenyatta alisema hivi karibuni ataisha mkubwa na wahudumu wa bodaboda ili kujadili mikakati ya kurejesha nidhamu na kunyoosha sekta hiyo.

“Hivi karibuni tutafanya mkutano nanyi ili tuweke mpango ambayo itatuwezesha kufanya biashara yetu huku tukiwaheshimu wanawake na tukitii sheria,”  akasema.

Kauli ya Rais Kenyatta ilijiri siku mbili baada ya Dkt Ruto na wandani wake kuishutumu vikali serikali kwa kile walichodai ni mpango wake wa kuwadhulumu wahudumu wa bodaboda.

Hii ni kufuatia msako ulioendeshwa na serikali hivi majuzi dhidi ya wahudumu wasiozingatia sheria kufuatia kisa ambapo baadhi ya wahudumu hao walimdhulumu mwanamke mmoja katika barabara ya Wangari Maathai, jijini Nairobi.

Akiendesha kampeni zake za urais katika mtaa wa Ngara, Nairobi, Jumatano, Dkt Ruto alitoa wito kwa waendeshaji bodaboda ambao pikipiki zao zilitwaliwa kwenda kuzichukua katika vituo vya polisi.

“Wahudumu wote wa ambao bodaboda zao zilichukuliwa na polisi waende katika vituo vya polisi wakazichukue. Aidha, warejeshewe faini ambazo walitozwa kinyume cha sheria, ili waendelee na biashara zao,” Dkt Ruto akasema.

Jumla ya wanabodaboda  17 walifikishwa mahakamani,  Nairobi kwa tuhuma za kumdhulumu mwanamke huyo ambaye ni afisa wa ubalozi wa Zimbabwe.

Mshukiwa mkuu wa unyama huo Zachary Nyaora Obadiah alikamatwa na polisi Jumatatu katika mji wa mpakani wa Sirare, akitaka kutorokea Tanzania.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending