Connect with us

General News

Rais Mstaafu Mwai Kibaki amefariki dunia – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Rais Mstaafu Mwai Kibaki amefariki dunia – Taifa Leo

TANZIA: Rais Mstaafu Mwai Kibaki amefariki dunia

NA MWANDISHI WETU

RAIS Mstaafu Mwai Kibaki aliyehudumu kati ya mwaka 2002 na 2013 amefariki dunia, ametangaza Rais Uhuru Kenyatta katika hotuba kwa taifa leo Ijumaa.

Kibaki alikuwa Rais wa Tatu tangu Kenya ijinyakulie uhuru mwaka 1963.

Rais Kenyatta amemtaja kama kiongozi aliyekuwa katika mstari wa mbele kuimarisha uchumi wa Kenya.

“Mwai Kibaki atakumbukwa kwa weledi wake na bidii yake kazini. Kwa mujibu wa mamlaka yangu kama Rais wa Kenya, ninaamuru kwamba bendera ya Kenya itapeperushwa nusu mlingoti nchini na katika balozi zote za Kenya katika mataifa ya kigeni kuanzia leo Ijumaa hadi Rais Mstaafu Kibaki atakapozikwa,” amesema Rais Kenyatta.

Kibaki aliingia ikulu kupitia kwa tiketi ya National Rainbow Coalition (NARC) na akaapishwa Desemba 30, 2002, kutumikia taifa kama Rais wa Tatu Jamhuri ya Kenya. Alihudumu kama kiongozi wa Taifa na Serikali hadi Aprili 9, 2013, alipokabidhi mamlaka kwa Rais Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta amesema japo taifa linaomboleza, lakini pia ni muhimu kukumbuka wakati ambapo Kibaki alitumikia taifa pamoja na wakati mzuri aliofurahia na mkewe Mama Lucy Kibaki ambaye naye alitangulia mbele ya haki 26 April 26, 2016, South Kensington, London, Uingereza.

Kibaki alizaliwa Novemba 15, 1931.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending