Akizungumza katika hafla ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe Charles Rubia katika Kaunti ya Murang’a mnamo Jumatatu, Desemba 30, Uhuru alisema serikali yake itatoa uhuru kwa Wakenya wote kama ilivyopiganiwa na viongozi waliotangulia.
“Hakuna mtu ambaye amezuiwa kusema yale anayotaka kusema. Ata nasikia kuna wengine wanataka kupanda ndege warudi..waendelee..hio ni uhuru wao,” alisema kiongozi huyo wa chama cha Jubilee.
Wakili Miguna anatazamiwa kuingia nchini Jumanne 7, Januari 2020. Source: UGC
Wakili huyo alitangaza kuwa atarejea nyumbani kupitia ukurasa zake za utandawazi siku ya Alhamisi, Desemba 19.
“Narejea nyumbani. Haki ya kuzaliwa, Haki ya Katiba na amri ya korti. Mabadiliko kwa ushawishi. Nitawasili: Jumanne, Januari 7, 2020 mwendo wa saa tatu na dakika 25 usiku kupitia ndege ya Lufthansa LH 590,” aliandika Miguna kwenye Twitter.
Wakili huyo alifurushwa kwa mara ya kwanza Februari 2018 baada ya kumuapisha kiongozi wa ODM Raila Odinga kama rais wa watu mnamo Jumanne, Januari 30 katika bustani ya Uhuru.
Mnamo Machi 2018, juhudi zake za kuingia nchini ziliambulia patupu huku serikali ikisema kwamba aliasi uraia wake wa Kenya ili kuwa raia wa Canada.
Huku akimjibu Uhuru, Miguna alisema kuwa atafuata sheria.
“Uhuru na haki za Wakenya kulingana na katiba ya Kenya ya 2010 inatakiwa kufurahiwa na kuendelezwa kwa uhuru bila kuathiriwa na Serikali. Hakuna atakaye wafunza Wakenya namna haki na uhuru zitatimizwa. Tutafanya hivyo kisheria,” aliandika Miguna mnamo Jumatatu, Desemba 19 mchana.
Hata hivyo, Wakenya walizua hisia mseto mtandaoni: