[ad_1]
Ruto ajitetea katika kesi ya kushinikiza apokonywe wadhifa
NA RICHARD MUNGUTI
NAIBU Rais Dkt William Ruto ameomba Mahakama Kuu itupilie mbali kesi ya watu wanaodai kuwa ni wapiganaji wa Mau Mau wakitaka atimuliwe mamlakani kwa madai ya kuacha kutekeleza majukumu yake.
Katika ushahidi aliowasilisha kortini, Dkt Ruto amesema kesi hiyo haina mashiko kisheria na lengo kuu ni kupotezea mahakama wakati.
“Mahakama Kuu haina mamlaka ya kutoa maagizo ya kumtimua kazini Dkt Ruto,” wakili Elias Mutuma alisema.
Wakili Mutuma alidokeza kwamba kesi hiyo haisimulii makosa yoyote ambayo Dkt Ruto alifanya ndipo afukuzwe kazini.
“Kesi hii dhidi ya Dkt Ruto haijawasilishwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo inastahili kutupiliwa mbali kwa vile hakuna ushahidi wa kumtimua,” akasema Bw Mutuma.
Kwenye kesi hiyo, kundi hilo linaomba mahakama imwachishe kazi Dkt Ruto likidai ameacha kutekeleza majukumu yake na kuanza harakati za kujipigia debe achaguliwe kuwa rais wa tano wa Kenya.
Pia wanaomba mahakama imtimue kazini Dkt Ruto kwa kuendeleza sera za chama cha United Democratic Alliance (UDA) ambacho hakikumdhamini wakati wa uchaguzi mkuu wa 2017.
Bw Kirungia amesema kuwa Dkt Ruto amekuwa akieneza mwongozo wa chama kingine mbali na chama cha Jubilee kilichomdhamini naibu wa rais katika uchaguzi mkuu wa 2017.
Next article
TAHARIRI: Sheria ya jinsia yafaa iangiliwe upya upesi
[ad_2]
Source link