Connect with us

General News

Ruto atumia jukwaa la mazishi ya Kibaki kunadi mfumo wa ‘bottom-up’ – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ruto atumia jukwaa la mazishi ya Kibaki kunadi mfumo wa ‘bottom-up’ – Taifa Leo

Ruto atumia jukwaa la mazishi ya Kibaki kunadi mfumo wa ‘bottom-up’

NA SAMMY WAWERU

NAIBU Rais Dkt William Ruto alitumia jukwaa la mazishi ya Rais mstaafu Mwai Kibaki Jumamosi kunadi sera zake za mfumo wa ‘bottom – up’.

Mzee Kibaki alizikwa nyumbani kwake kijiji cha Thunguri, Othaya, Nyeri katika maziko yaliyohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM, Raila Odinga, wanasiasa, viongozi wakuu serikalini, ndani na kutoka nje ya nchi.

Dkt Ruto ambaye anawania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 9, 2022, wakati akitoa rambirambi za pole amesema Rais Kibaki alitekeleza maendeleo na miradi chungu nzima na hivyo ni kiongozi wa kuigwa.

“Ikiwa kuna mfano unaofafanua mfumo wa bottom-up, tuusome kutoka kwa Mwai Kibaki,” Dkt Ruto akasema.

Rais Kibaki aliongoza Kenya kati ya 2002 na 2013, na Bw Ruto alihudumu kama waziri wa elimu na wa kilimo katika nyakati tofauti za utawala wake.

Ruto amesema ni chini ya Kibaki ambapo bei ya mbolea ilikuwa nafuu.

“Tufungue mianya ya ufanisi kwa watoto wetu katika kijiji hiki cha Thunguri na vijiji vingine Kenya, kama alivyotuhamasisha Rais Mwai Kibaki kwamba wanaweza kuwa watu wa maana nchini wakitia bidii na kumuomba Mungu,” Dkt Ruto akaambia waombolezaji.

Alipoalikwa jukwaani na Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Nyeri, Anthony Muheria kutoa rambimbi, watu walimshangilia.

Aidha, Ruto amekuwa akitumia mfumo wa kukwamua uchumi kutoka chini – mwananchi wa mapato ya chini, kuelekea juu, kusaka kura katika kampeni na jitihada zake kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

“Ninakubaliana na Balozi Francis Muthaura (aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma katika serikali ya Mzee Kibaki), Mwai Kibaki ndiye baba wa Kenya ya sasa. Ni ukweli,” akasisitiza.

Naibu rais pia alielezea kwamba Rais Kibaki alipanda mbegu ya mabadiliko ya Kenya kuwa bora, miundomsingi aliyoanzisha na inayoendelea kutekelezwa na rais wa sasa, Uhuru Kenyatta.

“Mzee Mwai Kibaki hakusahau mwananchi wa kawaida, na ndio maana chini ya utawala wake aliondoa ushuru unaotozwa pikipiki. Kwa sasa, sekta ya bodaboda imeajiri zaidi ya Wakenya milioni 1.4. Alikuwa Shujaa na aliyetangamana na raia kwa urahisi,” akafafanua.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending