Connect with us

General News

Sababu ya mizinga 19 kufyatuliwa badala ya 21 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sababu ya mizinga 19 kufyatuliwa badala ya 21 – Taifa Leo

Sababu ya mizinga 19 kufyatuliwa badala ya 21

NA WANGU KANURI

HAYATI Rais Mstaafu, Mwai Kibaki atapewa heshima ya mizinga 19 kabla ya kuzikwa nyumbani kwake Othaya, Kaunti ya Nyeri leo Jumamosi.

Mazishi ya Kibaki ndiyo ya tatu nchini kusherehekea kwa mizinga baada ya mtanguzli wake, Rais Daniel Arap Moi na Mzee Jomo Kenyatta ambaye alifariki akiwa madarakani 1978.

Sawa na Moi, Kibaki atafyatuliwa mizinga 19.

Kwa mujibu wa desturi za kijeshi, mmoja wao anapofariki akiwa kazini, yaani kabla kustaafu, anazikwa katika hafla ya kipekee ambapo mizinga 21 hufyatuliwa hewani, kuonyesha heshima kwa marehemu.

Hata hivyo, Rais Kenyatta anaweza kuamuru Kibaki kuzikwa na magwanda rasmi ya kijeshi kwa utendakazi wake kama rais kwa miaka kumi kati ya 2003 na 2013.

Ikiwa atazikwa na magwanda ya kijeshi, Kibaki atafyatuliwa mizinga 21 kwa heshima.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending