[ad_1]
Omicron: Safari 6,000 za ndege zafutiliwa mbali
Na MASHIRIKA
WASHINGTON, DC, AMERIKA
ZAIDI ya safari 6,000 za ndege zimefutiliwa mbali kote duniani tangu siku ya Krismasi, kulingana na tovuti maalum ya kutoa maelezo kuhusu safari za ndege.
Mashirika mengi ya ndege yalitaja hofu ya tishio la virusi vya Omicron kuwa sababu kuu ya kufutilia mbali safari hizo.
Nchini Amerika, hali mbaya ya hewa pia ilitajwa kuchangia hatua hiyo ya mashirika ya ndege.
Kulingana na tovuti ya Flightware.com, jumla ya safari 2, 800 zilifutiliwa mbali ama kuahirishwa kote duniani kama njia ya kudhibiti maambukizi ya aina hiyo mpya ya virusi vya corona.
Next article
Ukitaka kuvuna vinono kutokana na ufugaji wa ndege, tambua…
[ad_2]
Source link