General News
Sema kuachwa kwa mataa – Taifa Leo
Published
4 years agoon
By
Taifa Leo [ad_1]
Na THOMAS MATIKO
KUNA ngoma fulani ambayo Alikiba huimba kuhusu jinsi mapenzi yana-run dunia.
Zamani niliamini kauli hiyo lakini sio sasa.Sio katika karne hii tunayoishi ya 21. Enzi za wazazi wetu ni kweli mapenzi yali-run dunia ila kwenye kizazi cha sasa, watu wapo pamoja zaidi kwa kutegemeana na wala sio mapenzi.
Wiki iliyopita Nyota Ndogo alithibitisha kuwa kaachwa na yule mume wake mzungu Hunning Neilsen. Kuachwa na kuachana kupo, ila kile ambacho hunizengua ni jinsi ambavyo watu huachana au kuachwa hasa maceleb.
Wengine huwa hata hawapewi habari. Huwa wanashtukia tu wameachwa. Leo ninashuka na simulizi za mastaa kadhaa walioachwa kwa mataa na wapenzi wao bila ya kutarajia.
NYOTA NDOGO
Mkali huyu wa Watu na Viatu alifungua ndoa na mumewe Hunning Neilsen Mei 2016. Maisha yalikuwa mazuri tu hadi Aprili mwaka huu ambapo Nyota aliamka na kushtukia kaachwa na Nielsen hata bila ya kupewa taarifa.
Ngoma ilianza hivi, April 1, ikiwa ni siku ya Fools Day, Nyota aliamua kumzengua mumewe huyo, jambo ambalo linaonekana halikumfurahisha babu huyo ambaye kwa sasa yupo Denmark.
Siku hiyo, alimpigia simu na kumdanganya kuwa ni mjamzito. Neilsen aliguna na kisha kukata simu. Huo ukawa ndio mara yao ya mwisho kuwasiliana. Jamaa kawa mteja na kamlisha bloku Nyota kwenye namba zake zote hadi mitandaoni.
Nyota amejitahidi kuomba msamaha kwa utani huo lakini mpaka sasa bado mzee huyo hataki stori zake.
“Utani upo hata nao wazungu hufanya utani kutuliko sisi. Nahisi kuna jambo la ziada ambalo mimi silijui sababu nimejaribu kumfikia bila mafanikio. Binti yake mkubwa ni rafiki yangu sana na huwa tunazungumza sana. Nimejaribu kumfikia kupitia yeye ila aliniambia kila akizunguma na babake kisha ifikie kwangu, yeye huwa mkali. Hata ikitokea leo akataka nisafiri kwenda Denmark kuyamaliza, nitafanya hivyo bila kusita sababu nampenda sana,” alifunguka hivi majuzi redioni.
Nyota anasema walishakubaliana kwamba hawahitaji watoto zaidi na pengine ile taarifa yake kuwa ni mjamzito kidogo ilimshuta Nielsen ambaye umri wake unakaribia 80.
MEJJA
Okwonko alikuwa kwenye mahusiano mazuri tu na mpenzi wake aliyemzalia binti. Walijitahidi kuishi vizuri lakini siku moja alirudi nyumbani na kumkuta kaondoka.
“Hatukuwa tumekosana tulikuwa vizuri tu. Nakumbuka nilipofika Thika nikapata meseji akinuliza kama nimefika salama. Nilipomjibu ndio, alichoniambia ni kuwa, niendelee na maisha yangu bila ya kumuwaza yeye,” alifichua Mejja.
Wakati anaachwa, alikuwa amedumu kwenye penzi na mrembo huyo kwa miaka mitano na hata kuzaa naye.
Alimpata demu mwingine ambaye naye waliachana Disemba 2020 baada ya kuwa pamoja kwa miaka miwili. Demu wa pili angalau waliachana baada ya kufanya mazungumzo na kukubaliana kila mmoja ashike hamsini zake.
NADIA MUKAMI
Alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi aliyokuwa akiyafurahia. Kisha ikatokea mvutano kati yake na menejimenti yake ya zamani Hailemind Entertainment iliyoishia mahakamani.
Kulingana na Nadia mpenzi wake aliamua kumwachanisha kwa kuhisi kuwa penzi lao halikuwa likienda vizuri. Anasema zile drama za kortini ndizo zilimvuruga.
“Nilipokuwa na zile drama za mahakamani nilikuwa nikimpigia simu sana. Wajua nilikuwa mchanga na nilitaka kuzungumza na mtu ninayemwamini. Kuna siku nimempigia akaniomba nimpe muda kidogo atanipigia. Alipopiga baadaye alichoniambia ni kwamba tuvunje uhusiano wetu kwa sababu haukuwa ukimwendea poa. Nililia sana,” katiririka.
Nadia anasema hakutegemea kabisa kuachika kivile sababu hakukuwepo na ugomvi wowote baina yao kipindi hicho.
TERRY MUIKAMBA
Mtangazaji huyu wa redioni aliwahi kukiri kuachwa na jamaa kwa sababu alihisi kuwa ni mpole sana.
“Aliniambia mimi ni mstaarabu sana, sina drama kitu ambacho anapenda kiwepo kwenye mahusiano yake,” Terry alifichua 2019 akiwa hewani na akiwataka wasikikilizaji wake kusimulia visa vya kipuzi na kushangaza vilivyowapelekea wao kuachwa kwa mataa.
KAMENE GORO
Mtangazaji huyu wa Kiss 100 FM, aliolewa 2014 na Mtanzania mara tu baada ya kumaliza masomo yake ya shahada ya kwanza ya Uanasheria.
Alipata kazi kwenye runinga wakati huo na baada ya miaka michache ya kazi hiyo, mpenzi wake huyo akamtaka ahamie Tanzania baada yao kufunga ndoa kuanza maisha ya kuwa mke. Ni maisha aliyoyafurahia ingawaje wazazi wake hawakupenda
Anasema wakati mmoja akiwa amerudi Kenya kuwacheki wazazi wake, mume wake alimpigia simu na akamwambia ni bora tu waachane.
“Tulikuwa tunazungumza vitu vyetu vya kawaida na ni katikati ya maongezi hayo ndipo akaniamba anaona bora tuachane. Sikutegemea kabisa, nikamuuliza kama alikuwa na uhakika na anachokisema. Akanijibu ndio. Nilikata simu na sijawahi kuongea naye tena,” kafichua.
Kamene anasema alimpenda jamaa kweli sababu alikuwa akimjali na kumtunza vizuri na ndio sababu hakutegemea kuwa wangeishia kuachana kivile.
[ad_2]
Source link
Comments
You may like
Rayvanny officially leaves Diamond’s WCB Wasafi after 6 years

Raila Odinga is the most popular presidential candidate, a survey released by Infotrak

Newly-crowned Kenyan Wimbledon champion Angella Okutoyi would like to play against American star Serena Williams

The Mombasa High Court has ordered IEBC to clear Sonko to run for the Mombasa governorship.

A new born baby was pulled out of latrine in Mururi.

Kenyan Rapper Colonel Mustafa has leveled fresh accusations against his ex-girlfriend Katoto.

Okutoyi and Nijkamp qualify for Wimbledon Open final

Fans will have to brace themselves for a sober 90 minutes, the Gulf Arab state announces.

Angola’s longest ruler dos Santos dies at 79
