[ad_1]
Seneta aomba msamaha korti kuhusu chuki
NA RICHARD MUNGUTI
SENETA wa Nandi, Samson Cherargei (pichani) pamoja na wakili wake Dkt Duncan O’Kubasu, Alhamisi waliomba korti msamaha kwa kutofika kortini Aprili 18/19, 2022 wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya kueneza chuki.
Hakimu mkuu mahakama ya Milimani, Nairobi Wendy Kagendo alikubali msamaha wao na kuwaonya dhidi ya kutoheshimu korti.
Na wakati huo huo Dkt O’Kubasu aliagizwa afike mbele ya Jaji Grace Nzioka kuomba msamaha kutokana na matamshi yake ya kushusha hadhi ya mahakama.
Kiongozi wa mashtaka Alexander Muteti aliomba mahakama imkanye mshtakiwa dhidi ya kudharau korti na kesi inayomkabili.
Bi Kagendo aliamuru kesi iendelee Mei 19,2022 upande wa mashtaka utakapofunga ushahidi.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh500,000 pesa taslimu.
Next article
Sheikh akataa kutoka Kamiti
[ad_2]
Source link