[ad_1]
Polisi jijini Nairobi wanamsaka Seneta Johnson Sakaja kwa kukosa kujiwasilisha katika Kituo cha Polisi cha Kilimani baada ya kuachiliwa huru kwa dahamana.
Kama iliviripotiwa awali na TUKO.co.ke, Seneta Sakaja alikamatwa Jumamosi, Julai 18, mwendo wa saa nane mchana katika baa ya Ladies Lounge eneo la Kilimani kwa kukiuka sheria za kafyu.
Seneta huyo maarufu alipatwa akibugia pombe pamoja na marafiki zake na waliagizwa waondoke lakini walikataa na kuwataka polisi wawakamate.
Alikuwa mbishi na kutishia kuwahamisha maafisa wote wa polisi waliomkata kutoka Kituo cha Polisi cha Kilimani chini ya saa 24.
[ad_2]
Source link