Connect with us

General News

Serikali mbioni kuangamiza mbung’o waharibifu Kwale – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali mbioni kuangamiza mbung’o waharibifu Kwale – Taifa Leo

Serikali mbioni kuangamiza mbung’o waharibifu Kwale

NA SIAGO CECE

SERIKALI imeanzisha mpango maalumu wa kuangamiza mbung’o waliovamia Kaunti ya Kwale.

Mkurugenzi Mkuu wa baraza la kitaifa la kuangamiza mbung’o na kukabiliana na ugonjwa wa malale (KENTTEC), Bi Pamela Olet, alithibitisha wadudu hao wamevamia Mbuga ya Kitaifa ya Shimba Hills na maeneo jirani, na hivyo kuweka mifugo, binadamu na wanyamapori hatarini.

“Tunafanikiwa kutega takriban mbung’o 100 kwa kila mtego ndani ya saa 48 na tuna mitego kadhaa,” akasema.

Naye Mratibu wa KENTTEC eneo la Pwani Johana Cheptoo alisema kuwa wameanza mpango wa kuangamiza mbung’o ambao wameathiri kaunti zote sita za Pwani.

Kaunti iliyoathirika zaidi ni ya Kwale katika hifadhi ya Shimba Hills na msitu wa Bofu.

Alisikitika kwamba mbung’o hao wamesababisha vifo vya wanyamapori wengi kwa kuwanyonya damu na kusababisha ugonjwa wa malale.

KENTTEC imeshirikiana na Shirika la Kuhifadhi Wanyamapori (KWS) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (WRI) katika juhudi hizo za kuangamiza wadudu hao.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending