[ad_1]
Serikali yaongeza muda wa kusajili laini za simu hadi Oktoba 15
NA WANGU KANURI
TUME ya Mawasiliano nchini (CA) imeongeza muda wa usajili wa laini za simu kwa miezi sita.
Usajili huo uliokuwa umalizike jana sasa utaendelea hadi Oktoba 15, 2022 huku tume hiyo ikitishia kuadhibu kampuni za mawasiliano kwa kuzitoza faini iwapo Wakenya wanaotumia laini zao hawatakuwa wamezisajili.
Mkurugenzi Mkuu wa (CA), Ezra Chiloba Ijumaa alisema kuwa, nyongeza ya muda itawasaidia Wakenya wengi kujisajili.
Hata hivyo, Bw Chiloba alisema Wakenya ambao hawatakuwa wamezisajili laini zao wanajiweka katika hatari ya kufungwa jela kwa miezi sita au kulipa faini ya Sh300,000 au adhabu zote mbili.
Akizungumza Alhamisi katika eneo la Masol, kaunti ya Pokot Magharibi baada ya uzinduzi wa mradi, Chiloba alisema kuwa lengo la tume hiyo ni kukabiliana na matapeli wanaouza laini ambazo hazijasajiliwa.
Next article
Walioanguka mchujo UDA kutozwa hadi Sh200,000
[ad_2]
Source link