Connect with us

General News

Serikali yasema haitaingilia suala la karo – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Serikali yasema haitaingilia suala la karo – Taifa Leo

Serikali yasema haitaingilia suala la karo

Na KENYA NEWS AGENCY

SERIKALI haitawashurutisha walimu wakuu wa shule kuhusu utaratibu watakaotumia wanapoitisha karo kutoka kwa wazazi, Waziri wa Elimu katika Kaunti ya Nyeri, Sabina Aroni amesema.

Badala yake, usimamizi wa shule utahitajika kujadiliana na wazazi binafsi kuhusu mbinu wanazopanga kutumia kulipa masalio ya karo bila kutatiza uendeshaji wa huduma muhimu shuleni.

Bw Aroni alisema kuwa licha ya tangazo la hivi majuzi lililotolewa na Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha akishauri shule kutowafukuza wanafunzi kwa kukosa karo, mpangilio kama huo unaweza tu kufuatwa baada ya majadiliano ya kina baina ya wahusika.Alisema pesa bado ni kiungo cha kimsingi katika uendeshaji wa shughuli za taasisi za elimu.

“Shule zinahitaji pesa ili kuendelea na ikiwa wazazi hawatalipa tutaendeshaje shule zetu?” aliuliza afisa huyo.

“Ikiwa maji na umeme utakatwa, chakula kikose kulipiwa, hilo ni tatizo kuu na huo ni wajibu wa wazazi na walimu wakuu. Hatuingilii kamwe mpangilio huo na hivyo basi acha kuwe na maafikiano kuhusu ni vipi watashughulikia hayo,” alisisitiza.

Mwezi uliopita, Profesa Magoha aliwaagiza walimu wakuu wasiwafukuze wanafunzi kutokana na ukosefu wa karo lakini waunde mbinu watakayoafikiana kuhusu jinsi pesa hizo zitakavyolipwa.Waziri alisema haya katika Shule ya Sekondari ya Barani, Kaunti ya Kilifi.