– Watu 497 walipatwa na virusi vya Covid-19 Jumanne, Julai 14 baada ya sampuli 4922 kufanyiwa ukaguzi
– Watu watano wamefariki na kufikisha idadi ya walioangamizwa kuwa 202
– Serikali imetaka kusiwe na unyanyapaa dhidi ya wale ambao wameambukizwa virusi hivyo
Watu zaidi wanazidi kupatwa na maambukizi ya Coronavirus siku chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kufunguliwa kwa usafiri nchini.
Katibu Msimamizi katika Wizara ya Afya Mercy Mwangangi Jumanne, Julai 14 alisema watu 497 walipatwa na virus hivyo baada ya sampuli 4922 kufanyiwa ukaguzi.