[ad_1]
LISHE: Shayiri ya maziwa
NA MARGARET MAINA
[email protected]
SHAYIRI – oats – ni nafaka ambayo ni muhimu sana ikitumika kama chakula.
Kwa upande mwingine, shayiri ni malighafi muhimu katika utengenezaji wa sabuni na mafuta.
Uji wa oatmeal ni sehemu muhimu ya lishe ya binadamu. Kwa watoto ni muhimu kupika uji wa oatmeal tu kwenye maziwa maalum ya mtoto. Uji huu ni muhimu kwa sababu una kiwango cha juu cha mafuta na protini,huwa na asidi ya chini sana na hausumbui katika mfumo wa utumbo wa mtoto.
Lishe ya shayiri ina athari nzuri juu ya shibe hivyo unaweza kuzuia akili yako kuwaza chakula kila wakati. Hii ndio sababu shayiri ni nzuri kwa wanaotaka kupoteza uzani.
Ripoti ya Utafiti wa Kitaifa wa Afya na Lishe huko Amerika hata ilihitimisha kuwa ulaji wa shayiri husaidia kupunguza uzani.
Muda wa kuandaa: Dakika 5
Muda wa mapishi: Dakika 10
Walaji: 2
Vinavyohitajika
- oat flakes gramu 500
- sukari vijiko 3
- maziwa lita 1
- siagi vijiko 2
- chumvi
Maelekezo
Mimina maziwa kwenye sufuria na uiinjike kwenye jiko lenye moto hadi yachemke.
Koroga oat flakes kwenye sufuria yenye maziwa yaliyochemka.
Punguza moto na uanze kuyakoroga taratibu kwa dakika nane.
Angalie kwa makini kwamba haishikamani chini ya sufuria.
Baada ya dakika 10, epua na ufurahie.
Unaweza kumiminia juu njugu au vipande vya matunda kama ndizi au chochote ukipendacho.
Next article
Matajiri watesa maskini kwa ulafi
[ad_2]
Source link