Connect with us

General News

Shirika labuni teknolojia ya kuwasaidia watoto kusoma – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Shirika labuni teknolojia ya kuwasaidia watoto kusoma – Taifa Leo

Shirika labuni teknolojia ya kuwasaidia watoto kusoma

NA DAVID MUCHUI

SHIRIKA moja lisilo la kiserikali linatumia teknolojia kusajili na kuhakikisha wanafunzi katika kaunti kame hawakosi masomo.

Kenya Drylands Education Fund (KDEF), inapiga jeki elimu ya watoto wa wafugaji katika Kaunti za Marsabit na Samburu.

Bw Joseph Lesanjir, mwalimu katika kituo cha Elimu ya chekechea cha Nairabala (ECDE) eneo la South Horr, Kaunti ya Marsabit anasema yeye hutembea kilomita 26 kila siku kuenda na kutoka kazini.

Jambo muhimu zaidi kuhusu

safari yake ya kila siku ni kwamba imewawezesha wanafunzi wengi kati ya 41 waliomo katika kituo hicho kuendelea na masomo yao.

Kila asubuhi, Bw Lesanjir huwachukua watoto wengi njiani kuhakikisha wanafika darasani.

“Nilipoanza kazi hapa, niligundua kuwa watoto wengi walikuwa wakikosa kuenda shuleni mara kwa mara. Watoto walinieleza kuwa baadhi yao hawawezi kutembea safari ndefu kwa sababu wazazi wao wanatoka mapema kutafuta maji na malisho. Nisipowachukua asubuhi, wengi wao wataacha shule,” Bw Lesanjir anasema.

Umbali wa shule, unaoambatana na ukame, pamoja na mila na desturi za kitamaduni vimesalia kuwa vikwazo vikubwa kwa upatikanaji wa elimu katika maeneo mengi ya kaunti za Marsabit na Samburu.

“Wakati wa ukame, watoto hawawezi kuja shuleni ikiwa hakuna mpango wa kuwalisha.

Uhudhuriaji ni asilimia 100 wakati chakula kinatolewa shuleni,” asema Lesanjir.

Kituo hicho cha ECDE cha Nairabala, kilichoko umbali wa kilomita 13 Kaskazini mwa mji wa South Horr ni mojawapo ya vituo 10 vilivyojengwa na KDEF, kupiga jeki elimu ya watoto wa wafugaji katika kaunti za Marsabit na Samburu.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa KDEF Ahmed Kura, changamoto za kipekee zinazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa, utamaduni na ukosefu wa miundomsingi ya shule hufanya iwe vigumu zaidi kusajili na kuwahifadhi wanafunzi katika shule za maeneo kame.

Licha ya mipango ya serikali ambayo inahusisha kampeni za nyumba kwa nyumba za kuwafikia wanafunzi, idadi ya watoto wanaohusika katika ufugaji bado ni ya juu.

“Serikali ina uwezo wa kupata sajili ya shule ya kila siku lakini kuna mapungufu katika mawasiliano miongoni mwa washikadau. Hili ndilo pengo tunaloziba kupitia rejista ya shule ya kidijitali,” Bw Kura asema.

Katika makao yake yaliyoko Ngurunit, Kaunti ya Samburu, KDEF inatumia mfumo wa kidijitali uitwao EnART (Enrollment, Admission, Retention

and Transition), kufuatilia uandikishaji na mitindo ya mahudhurio ya shule kumi katika eneo hili.

“Programu hii ya kidijitali husaidia shule za msingi kufuatilia mahudhurio kwa utaratibu. Inafanya kazi pamoja na programu ya kukusanya data nje ya mtandao iliyoko kwenye kompyuta kibao. Mfumo huo unaweza kumfahamisha chifu wa eneo hilo na washikadau wengine husika ikiwa mwanafunzi ameacha shule au hayupo kwa zaidi ya siku 10,” Bw Kura aeleza.

Anasema zaidi ya wanafunzi 2,000 wanafuatiliwa kupitia mfumo huo.

“Chifu anapopewa taarifa anafaa kuwatafuta watoto hao na kuhakikisha wanarejea shuleni. Tumeona kuwa idadi ya watoto wanaosalia shuleni imeongezeka kutokana na hatua hiyo,” anasema.

Mbali na matumizi ya teknolojia, KDEF pia inaendesha mpango wa kulisha wanafunzi na usambazaji wa maji ili kupunguza athari za ukame.