Connect with us

General News

Simu za Sudi, Kositany zatwaliwa na DCI baada ya kuhojiwa saa kadha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Simu za Sudi, Kositany zatwaliwa na DCI baada ya kuhojiwa saa kadha – Taifa Leo

Simu za Sudi, Kositany zatwaliwa na DCI baada ya kuhojiwa saa kadha

NA ERIC MATARA

MBUNGE wa Kapseret, Oscar Sudi, mwenzake wa Soy Caleb Kositany na Spika wa Bunge la Uasin Gishu, David Kiplagat jana Jumapili waliachiliwa huru baada ya kuhojiwa na maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai (DCI) kuhusu kushambuliwa kwa kiongozi wa ODM Raila Odinga, kaunti ya Uasin Gishu, Ijumaa.

Hata hivyo, simu za watatu hao zilitwaliwa na maafisa hao baada ya mahojiano hayo yaliyodumu zaidi ya saa tano mjini Nakuru.

Helikopta ya Bw Odinga, ambaye ni mgombeaji urais wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya, ilishambuliwa kwa mawe na kuharibiwa na kundi la wahuni alipotoka nyumbani kwa marehemu Mzee Jackson Kibor, kufariji familia yake.

Kio ya helikopta hiyo kiliharibiwa kwa mawe katika kisa hicho kilichotokea hatua chache kutoka kwa boma la mwendazake, eneo bunge la Soy.

Magari ya viongozi walioandamana na Bw Odinga pia yaliharibiwa katika shambulio hilo linalodaiwa kutekelezwa na zaidi ya vijana 300.

Wanasiasa hao watatu waliwasili katika afisi za DCI ukanda wa Rift Valley, saa sita na dakika 56 za mchana jana Jumapili.

Walikuwa wakiitikia agizo la DCI lililotolewa Jumamosi baada ya wao kuhusishwa na upangaji pamoja na ufadhili wa shambulio hilo lilitokea Ijumaa jioni.

Spika Kiplagat, ambaye alikuwa amevalia jaketi ya manjano ndiye alikuwa wa kwanza kuhojiwa na maafisa wa DCI.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending