Connect with us

General News

Spika Mutura taabani – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Spika Mutura taabani – Taifa Leo

Spika Mutura taabani

NA RICHARD MUNGUTI

SPIKA wa Bunge la Kaunti ya Nairobi Benson Mutura alifikishwa kortini Ijumaa kwa wizi wa Sh5.3 milioni lakini hakusomewa shtaka hadi Mei 16, 2022.

Bw Mutura aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 na hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bi Esther Kimilu.

“Kulingana na agizo la Jaji Antony Mrima Bw Mutura hapasi kushtakiwa hadi kesi aliyowasilisha katika mahakama kuu isikilizwe na kuamuliwa,” Bi Kimilu alisema.

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda aliomba Bw Mutura asomewe mashtaka akisema mahakama kuu haijaamuru asishtakiwe.

Hakimu aliahirisha kesi inayomkabili hadi Mei 16, 2022 mahakama kuu itoe ufafanuzi wa agizo la Jaji Mrima.

Bw Mutura alilipa dhamana hiyo na kuondoka kizimbani mwendo wa saa nane.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending