– Sakaja na wenzake watatu walipatikana wakiburudika kwa vileo katika klabu ya Ladies Lounge saa za kafyu
– Alikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kilimani, aliachiliwa saa chache baadaye na akaagizwa kurejea saa tisa adhuhuri kuandikisha taarifa
– Sakaja alipuuzilia agizo hilo na kufanya maafisa wa polisi kumsaka hadi nyumbani kwake
– Seneta huyo sasa amejisalimisha katika kituo cha Kilimani na ameandikisha taarifa
Hatimaye seneta wa Nairobi Johnson Sakaja amejisalimisha katika kituo cha polisi cha Kilimani akiwa ameandamana na mawakili wake kuandikisha taarifa.
Sakaja alikamatwa Ijumaa, Julai 18 katika klabu ya Ladies Lounge saa nane usiku mtaani Kilimani akiburudika kwa vileo. Source: Twitter
Sakaja alifika katika kituo hicho Jumatatu, Julai 20 mwendo wa saa tatu asubuhi, saa kadhaa baada ya kukashifiwa kwa kukimbilia mafichoni.
Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, juhudi za kumfikia Sakaja kwa njia ya simu hazikufaulu na kuwalazimisha maafisa wa DCI kukikata kambi nyumbani kwake.
Baadaye, iligunduliwa kuwa seneta huyo alikuwa amefichwa nyumbani kwa mmoja wa viongozi wakuu serikalini katika mtaa wa Karen kwa ajili ya kuhofia usalama wake.
Sakaja alikamatwa Ijumaa, Julai 18 katika klabu ya Ladies Lounge saa nane usiku mtaani Kilimani akiburudika kwa vileo.