Connect with us

General News

Taratibu zote zifuatwe katika usahisishaji mitihani watahiniwa wapate haki – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Taratibu zote zifuatwe katika usahisishaji mitihani watahiniwa wapate haki – Taifa Leo

WANTO WARUI: Taratibu zote zifuatwe katika usahisishaji mitihani watahiniwa wapate haki

NA WANTO WARUI

WAZIRI wa Elimu, George Magoha wiki jana alitangaza kuwa, matokeo ya mtihani wa Darasa la Nane (KCPE) yatatangazwa ndani ya majuma mawili yajayo.

Alisema mtihani ulianza kusahihishwa punde tu Taasisi ya Mitihani Nchini (KNEC) ilipopokea mitihani iliyofanywa siku ya kwanza.

Waziri alisema mashine za kusahihisha mitihani kwa haraka zitarahisisha kazi hiyo ya usahihishaji akisema ni za kisasa.

Utendakazi wa aina hii ni mzuri na wa kupongezwa na kila Mkenya.

Unaondoa nafasi ya utepetevu na kupunguza kuchokorwa kwa alama na watu wasiopenda maendeleo.

Kwa muda mrefu, mitihani ilikuwa ikichukua siku nyingi kabla ya kutangazwa huku watahiniwa wakisubiri kwa wasiwasi mwingi.

Katika muda huo wote, kuna uwezekano matokeo hayo yalikuwa yakibadilishwa ili kuwafaa baadhi ya watu.

Ingawa hatua hii ya kutangaza mitihani haraka ni muhimu na ya kutia moyo, ipo hatari ya kutoa matokeo yenye kasoro hapa na pale kama ilivyowahi kufanyika awali.

Matokeo yanapoachiliwa yakiwa na kasoro, jambo hilo huwaathiri wahasiriwa kwa muda mrefu hata baada ya kurekebishwa.

Hii ndiyo sababu KNEC inastahili kuwa na uangalifu mkubwa kabla ya kutoa na kutangaza matokeo ya mitihani.

Wanachi hasa wazazi na wanafunzi waliofanya mtihani wa KCPE wanatarajia kupata matokeo yanayolingana na bidii na uwezo wa wanafunzi hao.

Mara kwa mara, matokeo ya mitihani yamesababisha hasara kubwa kwa baadhi ya wananchi ikiwemo wanafunzi wengine kujitoa uhai.

Licha ya kuwa usawazishaji wa alama unaofanywa na KNEC ni muhimu, unafaa kufanywa kwa uwajibikaji mkubwa bali si kwa uonevu wa aina fulani.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending