Akizungumza na TUKO.co.ke, dada yake marehemu, Elizabeth Keige alisema aliaga dunia siku ya Jumanne, Julai 7 mchana, na sasa wanafanya mpango wa kumzika Jumanne, Julai 14.
Atazikwa katika hafla ya faragha itakayoandaliwa nyumbani kwake Muruka Kandara, kaunti ya Murang’a.
Kulingana na wajiriwa, Keige alikuwa amekula chakula cha mchana wakati aliamua kutembea na kisha kuzirai nje ya nyumba yake, kama ilivyoripoti The Standard.
“Mdosi alikuwa tu amemaliza kula chakula cha mchana wakati aliamua kuenda mazoezi.Hatua chache kutoka kwa lango lake, alizirai,” alisema mmoja wa wafanyakazi wake.
Kufuatia kifo chake, kulikuwa na uvumi kwenye mitandao jamii kuwa huenda alifariki kutokana na COVID-19 lakini daktari wake alizima uvumi huo akisema tajiri huyo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Hoteli ya Tavern, iliyoko katika Barabara ya Ngong, jijini Nairobi, imekuwa ikigonga vichwa vya habari kwa muda kufuatia madai kuwa ilikataa kukubali kundi la wasiomuamini Mungu siku ya wikendi ya Pasaka.
Klabu hicho kinasifika kwa huduma zake bora kutoka kwa wahudumu wake.
Tavern ina vumba vya mikutano, hoteli, baa na baadhi ya sehemu ya kuandaliwa hafla mbali mbali kama vile Jiweke Sundays na Jiweke Furahidays.