Connect with us

General News

Timu za voliboli ya ufukweni zawasili nchini Ghana kusaka tiketi ya Madola – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Timu za voliboli ya ufukweni zawasili nchini Ghana kusaka tiketi ya Madola – Taifa Leo

Timu za voliboli ya ufukweni zawasili nchini Ghana kusaka tiketi ya Madola

NA JOHN KIMWERE

TIMU za taifa za voliboli ya ufukweni upande wa wanaume na wanawake zimeondoka leo Jumatatu alfajiri kuelekea jijini Accra, Ghana ambako zimeshawasili ili kushiriki mechi za kuwania tiketi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola.

Shindano hilo litafanyika Machi 24 hadi 29.

Timu za wanawake zitakosa huduma za wachezaji wawili, Phosca Kasisi na Yvonne Wavinya walioshiriki Michezo ya Olimpiki nchini Japan mwaka 2021.

Wawili hao walitemwa baada ya mchezo wao kudidimia.

”Kama nilivyoahidi hatuendi kutalii nchini Ghana bali nia yetu itakuwa kushinda tiketi ya kuwakilisha bara la Afrika,” kocha wa timu za wanaume, Patrick Owino alisema na kuongeza hata hivyo wanafahamu haitakuwa mteremko hivyo lazima wajitume.

Meneja wa vikosi hivyo, Sammy Mulinge anashikilia kuwa ana imani wachezaji hao wamekaa vizuri kukabili wapinzani wao.

”Tunaamini tumeshiriki mazoezi ya kutosha na wachezaji wapo fiti pia tayari kushiriki ngarambe hiyo,” alisema.

Kipute hicho kitashirikisha Nigeria, Msumbiji, Gambia na wenyeji Ghana.

Timu za wanaume zinajumuisha: Nicholas Lagat, Donald Mchete, Ibrahim Odour na James Mwaniki huku wanawake wakiwa: Veronica Adhiambo, Naomi Too, Brackcides Agala na Gaudencia Makokha.

Wengine katika ujumbe huo ni; Salome Wanjala (kocha wa timu za wanawake), Sammy Mulinge (meneja), Mzinga Kyalo (refarii) na daktari Sarah Karongo.